LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 18, 2021

ANZISHENI TRENI KATIKA MIJI INAYOKUA, KAMILISHENI BARABARA BUSANDA -MBUNGE MAGESA

 Mbunge wa Busanda, Bryceson Magessa ametoa ushauri kwa Serikali kuwa na mpango wa kuanzisha Treni za umeme zitakazotoa huduma kwenye miji inayokuwa (Mfano Treni inayotoa huduma kati ya Tazara hadi Mwakanga Dar es Salaam maarufu kama Treni ya  Mwakyembe) kuliko kuingia gharama kubwa ya kujenga barabara na kuanzisha miradi ya Mabasi yaendayo Haraka ambayo inagharama kubwa ya uendeshaji.

Aidha Mbunge Magessa ameiomba serikali kukamilisha miradi ya ujenzi wa barabara ambayo imekwama kwa muda mrefu katika jimbo lake la Busanda ili kuwanguzia kero wananchi.

 Mbunge Magessa ametoa ushauri  huo alipokuwa akichangia Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakati wa Mkutano wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kikao cha 29, Mei 17,2021 jijini Dodoma. 

 

Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Magesa akitoa  ushauri huo.....

 

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM

 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages