Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa uchumi wa Zanzibar unakua kwa kasi zaidi ambapo kwa mwaka huu umeongezeka hadi kufikia asilimia 7.1 na kwa upande wa Tanzania Bara unakua kwa asilimia 6.
Dkt. Samia amebainisha hilo, alipokuwa akihutubia katika mkutano wa Kampeni zake kwenye Uwanja wa Hamburu, Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar, Septemba 18, 2025.
Amesema kuwa usinamizi mzuri wa sera za kiuchumi na kifedha ndiyo uliosababisha uchumi huo kukua kwa upande wa Zanzibar.
Amesema kuwa kabla ya janga la Covid na kuporomoka kiuchumi, Tanzania Bara uchumi wake ulikuwa unakua kwa asilimia 7 na kwamba mwakani 2026 na 2027 utafikia kama wa Zanzibar asilimia 7.
Amesema matokeo hayo yamewezesha ujenzi wa shule nzuri za ghorofa, masoko, hospitali za kisasa, barabara na miradi mingine ya maendeleo. Pia uchumi wa wananchi wa Zanzibar umekua.



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇