Wednesday, February 20, 2019

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.SHEIN AWASILI KISIWANI PEMBA JIONI LEO KUAZA ZIARA YAKE YA KISERIKALI KESHO

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman Abdallah,alipowasili Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume Chakechake Kisiwani Pemba leo jioni, kwa ajili ya Ziara yake ya Kiserikali inayotarajiwa kuaza kesho kutembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Wananchi alipowasili Uwanja wa Ndege wa Karume Chakechake Pemba, leo jioni  kwa ajili ya ziara yake ya Kiserikali kwa Mikoa miwili ya Kusini na Kaskazini Pemba inayotarajiwa kuaza kesho.(Picha na Ikulu)
Share:

RAIS DK. MAGUFULI AFANYA UTEUZI

Share:

RAIS DK. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA OFISA MWENDESHAJI MKUU WA KAMPUNI YA BARRICK GOLD CORPORATION, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Willem Jacobs, alipokutana naye na kufanya  mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam, leo Februari 20, 2019
Rais Dk. John Magufuli akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga wakati wa mazungumzo yake na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Willem Jacobs na ujumbe wake, Ikulu jijini Dar es salaam, leo. 
Rais Dk. John Magufuli na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga wakiwa katika picha ya pamoja  na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Willem Jacobs na ujumbe wake baada kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 20, 2019.
Rais Dk. John Magufuli akiagana na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Willem Jacobs baada ya  kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 20, 2019 (Picha na Ikulu)
Share:

TRUMP ACHUNGUZWA KUTAKA KUIUZIA SAUDI ARABIA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA

Donald Trump Mohammed bin Salman Saudi Arabien (picture alliance/dpa/M.Wilson)
Bunge la Marekani tayari limeshafungua uchunguzi dhidi ya pendekezo la utawala wa Trump, la kutaka kujenga vituo kadhaa vya kinyuklia nchini Saudi Arabia.
Mwakilishi Elijah Cummings, mwenyekiti wa Kamati ya Halmashauri ya Uangalizi na Mageuzi, ameitaka Ikulu ya Marekani kuwasilisha nyaraka ikiwa zile zinazohusu mkutano uliofanyika miezi miwili tu baada ya Trump kuingia madarakani kati ya mkwewe, Jared Kushner, na mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia , ambae muda mchache baada ya mkutano huo alitangazwa mrithi wa ufalme wa nchi hiyo ya Kiarabu.
Ripoti ya Kamati ya Uangalizi ya Baraza la Wawakilishi imesema mshauri wa zamani wa usalama wa taifa Michael Flynn na wenzake wawili walipendekeza mpango huo kwa Tom Barrack, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya kuapishwa kwa rais, na muungano wa makampuni ya Marekani yakiongozwa na makamanda wa kijeshi waliostaafu na viongozi wa zamani wa Ikulu ya Marekani.
Juhudi za mpango huo, ripoti imesema zilianza kabla ya Trump kuingia madarakani na kuendelea hadi baada ya kuapishwa kwake Januari 2017, licha ya wafanyakazi wa Baraza la Usalama wa Taifa kuonya kwamba uhamisho wa teknolojia ya nyuklea ya Marekani kwenda Saudi Arabia unaweza kuangaliwa kama uvunjaji wa Sheria ya Nishati ya Atomiki.
Saudi Arabien - Präsident Trump zu Besuch (picture-alliance/abaca/Balkis Press)
Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdelaziz, wakati wa ziara yake katika taifa hilo la kifalme.
Wabunge wamtaka Trump akae mbali na Salman
Mwanasheria wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la taifa John Eisenberg, aliamuru mpango huo usitishwe kwa sababu ya wasiwasi huenda Flynn akawa anavunja sheria kutokana na mgongano wa maslahi, kwa vile alikuwa mshauri wa muungano wa makampuni hayo yatakayofaidika na mpango huo, huku akiwa bado anatumika katika kampeni ya Trump na timu yake ya mpito. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti hiyo, ambayo imetumia ushahidi wa nyaraka tofauti na maelelezo ya watu waliofichua siri.
Ripoti hiyo imeongeza kwamba, uungwaji mkono kutoka katika serikali ya Trump hata hivyo unaendelea hado hivi karibuni, huku Trump akionekana wiki iliyopita kukutana na wawakilishi wa makampuni yanayotarajiwa kufaidika na mpango huo, katika ofisi yake ya Ikulu.
Wabunge wa Marekani, wakiwamo wa chama cha Trump cha Republican, wamekuwa wakiishinikiza Marekani kujiweka mbali na mwanamfalme Mohammed bin Salman kufuatia mauaji ya mwanahabari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi. yanayodaiwa kuongozwa na taifa hilo la kifalme. Pia wanaitaka serikali ya Marekani, kusitisha kuviunga mkono vita vya Yemen, ambako mamilioni ya watu wako hatarini kutumbukia katika janga la njaa katika kile Umoja wa Mataifa inachokieleza kama mgogoro mbaya wa kibinadamu kushuhudiwa ulimwenguni.
Mwandishi: Yusra Buwayhid/afap,rtre
Share:

RUGE MUTAHABA NDIYE ALIYE NISHAURI KUTEMBEA PEKUMsanii wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto amesema mtindo wake wa kutembea bila viatu ulikuja baada ya kushauriwa kufanya hivyo na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media, Ruge Mutahaba.

Mpoto ametoa siri hiyo wakati akihojiwa na mtangazaji katika kipindi cha Clouds 360 kwenye Kituo cha Televisheni cha Clouds TV na kuongeza kuwa Ruge pia amechangia sana kumtengeneza kisanaa.

"Aliniambia tayari wewe unaimba mashairi je unataka watu wakupambanuaje?, nikamwambia nitavaa magunia akasema sawa hiyo haitoshi ongezea nyingine”

Ameendelea kwa kusema kuwa, 'Ni Ruge aliyenitengeneza mimi kuwa tofauti kwa mashairi yangu, mwanzoni nilikuwa naimba tu kikubwa zaidi alinitengeneza yaani kuni-brand,'
Share:

WAZIRI MKUU AAGIZA KUIMARISHWA ULINZI MIPAKANI KUKABILINA NA ONGEZEKO LA VITENDO VYA UHLIFU


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi na doria katika maeneo ya mipaka kutokana na ongezeko la vitendo vya mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha na vitisho kwa wananchi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wilayani Kibondo wakati akihitimisha ziara yake mkoani Kigoma.

“Kulinda usalama wa nchi ni jukumu letu sote na si la vyombo vya ulinzi na usalama pekee, kila mmoja anapaswa kushiriki. Kwa upande wa majirani zetu wanaotaka kuja nchini ni lazima wafuate taratibu kwa kuomba vibali.” amesema Waziri Mkuu.

Pia, Waziri Mkuu ameagiza wakimbizi wote watakaobainika kutoroka kwenye makambi wanayohifadhiwa na kuingia uraiani wakamatwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za Tanzania, kwani wanachokifanya ni ukiukwaji wa sheria.

Share:

MAGAZETI YA LEO 20/2/2019
Share:

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWAONYA WANAOFANYA USAFIRISHAJI KWA NJIA YA MAGENDO

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein amewataka Wananchi wanaojishughulisha na vitendo vya usafirishaji kwa njia za magendo kuacha tabia hiyo vyenginevyo sheria itachukua mkondo wake.
Sheria hiyo inaelekeza Mali iliyosafirishwa kwa njia ya magendo pamoja na Chombo kilichohusika kusafirishia kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Dk. Shein alitoa kauli hiyo wakati akiwahutubia Wananchi wa Uzi Ng’ambwa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua shughuli za Serikali na Chama mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema tabia ya kusafirisha bidhaa kwa njia ya magendo ni mbaya kwani huikosesha Serikali mapato  ambayo hutumika katika kuendeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Amekiomba Kikosi cha kuzuia magendo Zanzibar KMKM kufanya kazi zake ili kuhakikisha biashara hiyo inakoma katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
“Ndugu zangu nakuombeni sana jiepusheni sana na Magendo, Kikosi chetu cha KMKM tumekiwezesha kwa vifaa, hivyo anayejaribu kufanya magendo atakamatwa tu na kufilisiwa” alitanabahisha  
Akizungumzia kuhusu huduma ya maji safi na salama katika Kisiwa hicho Dk Shein amesema Serikali imejipanga vyema kuhakikisha huduma hiyo inapatikana muda wote.
Amesema kwa sasa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati inaendelea na mipangilio yake kuhakikisha kunajengwa Tangi la Maji ambalo litatumika kusambazia huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Uzi.
Kuhusu huduma ya usafiri wa kufikia kisiwani hapo Dk Shein amesema Serikali ina mpango wa kujenga Daraja litakalowezesha Wananchi kufika katika kisiwa hicho kwa wepesi.
Daraja hilo litaanzia katika Kijiji cha Ungujaukuu Kaipwani hadi Uzi na kujengwa juu ya usawa wa bahari ili kusaidia wananchi kufika kisiwani huko muda wote.
Katika kutekeleza azima hiyo Serikali itaomba Mkopo katika Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya Kisiwa cha Uzi.
“Nakuombeni vuteni subra, Serikali ipo kwa ajili ya kukuleteeni maendeleo tumeshajenga miradi mingi ya gharama, hivyo Daraja haliwezi kutushinda tutalijenga panapo majaaliwa” alibainisha Dk. Shein.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kati Mashavu Said Sukwa ameelezea mafanikio ya Wilaya yake ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo mbali mbali vya Wilaya hiyo.
Aidha ameishukuru Serikali kwa hatua yake ya kufanya ugatuzi jambo ambalo limesaidia kuzikabili changamoto za Wilaya.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Juma Abdallah Sadala ameipongeza Wilaya hiyo kwa mashirikiano mazuri katika ya Viongozi wa Serikali na Chama hali inayopelekea kasi ya maendeleo Wilayani humo.
Amewapongeza Wananchi na Wanachama wa Wilaya ya Kati kwa kubuni miradi ya maendeleo ambayo husimamiwa vyema na Serikali.

Hivyo amewaomba Wanachama kuendelea kushirikiana vyema na viongozi wao ili kutekeleza vyema Ilani ya CCM ya mwaka 2015-20.
Reply
Reply all
Forward
View Gmail in: Mobile | Older version | Desktop
© 2018 Google
Share:

MWANAMKE AJIFUNGUA WATOTO SABA KWA MPIGO


Mwanamke nchini Iraqi, amejifungua watoto saba kwa mpigo, hali inayoelezwa kuwa ni miongoni mwa miujiza iliyowahi kutokea duniani.

Mwanamke huyo aliyejifungua salama kupitia njia ya kawaida, anasemekana kuwa katika hali nzuri kiafya na watoto wake pia wapo katika hali nzuri.

Kulingana na ripoti ya Daily Mail, mwanamke huyo aliyejifungulia katika mkoa wa Diyali ni wa kwanza kujifungua idadi hiyo ya watoto nchini humo.

 Msemaji wa hospitali alimojifungulia mama huyo alithibitisha tukio hilo na kusema kuwa, aliwasili katika hospitali hiyo na kujifungua watoto sita wa kike na mmoja wa kiume. 

Baba wa watoto hao Youssed Fadl, alisema yeye na mke wake hawakutarajia idadi hiyo ya watoto na sasa wana watoto kumi wa kulea, wakiwamo wa mbeleni.

 Pia Fadl alisema mke wake hakuwa na ufahamu angeweza kupata watoto zaidi ya mmoja kabla ya kuupata ujauzito huo. © Malunde Blog
Share:

Tuesday, February 19, 2019

RAIS DK. MAGUFULI AMTUMBUA MKURUGENZI WA PSSSF, ATEUA MWINGINE KUSHIKA NAFASI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Februari, 2019 amemteua Hosea Ezekiel Kashimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (Public Service Social Security Fund – PSSSF).Kashimba anachukua nafasi ya Eliud Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo Kashimba alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wengine 2 kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Augustine Emmanuel Mbokella kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya TIB (TIB Corporate Bank Limited).

Na pili, Rais Magufuli amemteua Latifa Mohammed Khamis kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara za Nje (TANTRADE).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza leo tarehe 19 Februari, 2019.
Share:

VYUO VIKUU VYA AFYA MBIONI KUTUMIA MTAALA MMOJA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS), Taaluma, Utafiti na Ushauri Profesa Appolinary Kamuhambwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mradi wa kufikia walengwa katika mageuzi ya Utoaji Elimu ya fani za Afya Tanzania, katika ukumbi wa MUHAS Dar es Salaam, leo.

NA KHAMISI MUSSA
 Vyuo Vikuu vya Afya na Sayansi Shirikishi hapa nchini vinatarajiwa kuanza kutumia mtaala mmoja kufutia kupatikana kwa mradi mpya wakuwafikia walengwa katika mageuzi ya Utoaji Elimu ya fani za Afya.  

Hayo yamesemwa leo na Mtafiti mkuu wa mradi huo Profesa Ephata Kaaya katika Uzinduzi wa mradi huo ambao umefadhiliwa na Shirika la Afya la Marekani.

Katika uzinduzi huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Jijini Dar es Salaam Profesa Kaaya ambaye ni Makamu Mstaafu Chuo hicho alisema mradi huo unalenga kuwafikia walengwa katika Mageuzi ya Utoaji Elimu ya fani za Afya hapa nchini.

Alisema mradi huo utaanza kuboresha zaidi elimu ya afya katika vyuo vya MUHAS, KCMC Bugando na baadaye katika vyuo vyote nchini hali itakayo wezesha kutotohautiana kwa mitaala katika vyuo vyote nchini

"Kilichofanyika hapa ni kufungua kuanza kwa wakati wa mradi huu uliofadhiliwa na Shirika la Afya la Marekani  ambapo kazi yake kubwa ya huu mradi ni kuboresha Ufundishaji wa Elimu za afya na kuboresha mtaala kwa ufanisi zidi na uboreshaji wa walimu" alisema Profesa Kaaya.

Alisema hatua hiyo baadaye itawezesha kupatikana wataalam wa afya wenye kuweza fanya kazi kwa umahiri kuliko ilivyo sasa na kufafanua kuwa wakati wa kufanya kazi 
katika mradi huo watakuwa wakishirikishwa wadau wote na ikiwemo mabaraza ya taaluma za afya  kama TCU na wadau wengine wote wakiwemo walimu na wanafunzi.
Mtafiti Mkuu wa Mradi wa kufikia walengwa katika Mageuzi ya Utoaji Elimu ya fani za Afya Tanzania, Profesa Ephata Kaaya akizungumza na wadau wakati wa uzinduzi wa mradi huo, katika ukumbi wa MUHAS Dar es Salaam, leo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
PICHA ZAIDI>BOFYA HAPA


Share:

SERIKALI YAMALIZA SAKATA LA MAKONTENA YALIYOKWAMA BANDARINI DAR
Serikali imetatua kadhia ya makontena ya wafanyabiashara wa DRC kukwama Bandarini, Dar es Salaam na sasa makontena hayo yameanza kutoka Bandarini.

Waziri Kamwelwe amesema makontena hayo yalizuiwa baada ya kujitokeza tena tuhuma za baadhi ya wa wafanyabiashara kubakiza nchini bidhaa zilizopaswa kwenda nje ya nchi.Kaimu Balozi wa DRC nchini naye amemshukuru Rais Magufuli na Waziri Kamwelwe kwa kulimaliza tatizo lililojitokeza katika taratibu za forodha na ameahidi atasimamia wafanyabiashara wa DRC kufuata sheria za nchi.


Share:

RUGE MUTAHABA APACHIKWA JINA LA 'RUGE THE FIGHTER AFRIKA KUSINI'Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano, January Makamba amesema alipata nafasi ya kwenda Afrika Kusini kumuona Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kinachoruka Clouds TV ambapo ameeleza Madaktari wanaomtibu Ruge wamempa jina la mpambanaji kutokana na namna anavyoumwa.

"Mimi nilipata nafasi ya kwenda South Afrika, nikaamua nikawaone madaktari wake, wamempa
jina wanamuita 'RUGE THE FIGHTER," amesema Waziri Makamba.

Katika hatua nyingine, amesema Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Mwaka 2015, hakuhusika katika mchakato wa utungwaji kwa sababu alikuwa Naibu Waziri Mawasiliano, na mchakato ulihusisha wataalamu wa wizara, makatibu wakuu, mawaziri, na yeye hakuwa miongoni mwa makundi hayo.
Share:

MWANAMAMA MCHINA JELA MIAKA 17 KWA KESI YA MENO YA TEMBO

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam,  leo asubuhi imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 17 jela baada kumtia hatiani Mwanamke raia wa China, Yang Feng  Glan waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya meno ya tembo yeye na wenzake wawili.

Hukumu hiyo imesomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye amesema Jamhuri wamethibitisha, ushahidi inajitosheleza kwamba washtakiwa walitenda makosa hayo.

Hakimu Shaidi aliwatia hatiani na kusema kwamba walifanya dharau kubwa kutumia maroli ya Serikali kubebea meno ya tembo kupeleka bandarini.

Alisema Mahakama ilifika katika shamba Muheza Tanga ambapo mshtakiwa wa pili alikuwa analima pilipili na humohumo ndiko walikokuwa wanafukia meno ya tembo, wanafukua na kuyasafirisha Dar es Salaam.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni raia wa China, Yang Feng Glan(66), Salvius Matembo Philemon Manase Katika kesi hiyo upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi 11 wa upande wa utetezi, washtakiwa walijitetea wenyewe.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na biashara haramu ya Meno ya Tembo yenye thamani ya Sh bilioni 13 kinyume cha sheria.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao, wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa katika kipindi hicho walifanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889, vikiwa na thamani ya Sh bilioni 5.4 bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.
Share:

RAIS WA NIGERIA AWATAKA POLISI NA WANAJESHI KUTOONYESHA HURUMA KWA WEZI WA KURA


Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amewaamuru polisi na wanajeshi nchini humo wasionyeshe huruma mbele ya wezi wa kura kipindi hiki wakati maandalizi yakiendelea kwa ajili ya uchaguzi huo ulioahirishwa.

uchaguzi Mkuu nchini Nigeria unatarajiwa  utafanyika Jumapili ijayo February 23, 2019, mara baada ya Tume huru ya uchaguzi nchini humo (INEC) kuhahirisha hapo February 16 mwaka huu.

INEC walitangaza kuhairishwa kwa uchaguzi huo saa tano tu kabla ya wapiga kura kuelekea katika vituo vya upigaji kura.

Hata hivyo vyombo vya habari vya ndani nchini Nigeria viliripoti kuwa vifaa vya kupigia kura vilikuwa bado havijawasili katika maeneo yote nchini humo.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

CCM Blog. Powered by Blogger.