LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 17, 2026

WAZIRI HOMERA AZINDUA “SEMA NA WAZIRI” KUIMARISHA HUDUMA ZA KISHERIA

 Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Zuberi Homera, amezindua rasmi programu ya “Sema na Waziri” leo Machi 17, 2026 jijini Dodoma, ikiwa ni hatua mpya ya kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za kisheria nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Homera amesema kuwa programu hiyo inalenga kuwapa Watanzania fursa ya kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja kwa Waziri na kupatiwa ufafanuzi wa haraka kuhusu masuala ya kisheria yanayowakabili.

Uzinduzi huo uliambatana na tukio la Waziri kupokea simu za moja kwa moja kutoka kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini, akisikiliza kero zao na kuzitolea majibu papo hapo.

Amesema kuwa huduma ya “Sema na Waziri” inatarajiwa kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi kwa kuwawezesha kufikisha malalamiko yao kwa urahisi zaidi na kuyapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Aidha, imeelezwa kuwa programu hiyo itaongeza ufanisi katika utatuzi wa migogoro ya kisheria na kuonesha namna Serikali inavyojali na kusikiliza wananchi wake.

 “Uzinduzi wa programu hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akihimiza viongozi wa umma kusikiliza wananchi na kuhakikisha wanapata haki zao kwa wakati.”amesema Dkt.Homera

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amesema kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ilianzisha Kituo cha Huduma kwa Mteja mwaka 2024 kama sehemu ya kuboresha huduma, na kwamba uzinduzi wa “Sema na Waziri” ni mwendelezo wa juhudi hizo za kuimarisha upatikanaji wa haki kwa Watanzania.

Amebainisha kuwa hadi sasa jumla ya malalamiko 2023 yamepokelewa, ambapo kati ya hayo, 1394 tayari yamepatiwa ufumbuzi huku mengine yakiendelea kufanyiwa kazi ili kupata suluhisho la kudumu.

Katika moja ya simu zilizopokelewa, mwananchi kutoka Geita aliuliza kuhusu lini mchakato wa Katiba mpya utakamilika. Akijibu swali hilo, Waziri Homera alisema:

“Mchakato wa Katiba ni wa wananchi na ni sehemu ya Ilani ya CCM. Kwa sasa tunasubiri hatua zinazoendelea chini ya Rais, hivyo ni vyema kuwa na subira kwani jambo hili halijaachwa.”

Kwa ujumla, uzinduzi wa programu ya “Sema na Waziri” unaashiria hatua muhimu katika kuimarisha utawala bora, uwazi, na upatikanaji wa haki kwa wananchi wote nchini.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Zainabu Katimba, amesema kuwa uzinduzi wa programu ya “Sema na Waziri” ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliyelitaka Serikali kutumia mifumo ya TEHAMA ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Katimba ameeleza kuwa matumizi ya teknolojia yatawezesha wananchi wengi zaidi kufikia huduma za kisheria kwa urahisi, bila kulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.

 “kupitia programu ya “Sema na Waziri”, wananchi watapata fursa ya kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja na kupatiwa majibu pamoja na ushauri wa kisheria kwa wakati, jambo litakalosaidia kupunguza migogoro na kuongeza uelewa wa sheria katika jamii.”amesema Mhe.Katiba

Aidha, amebainisha kuwa kituo cha huduma kwa mteja cha Wizara ya Katiba na Sheria kitaendelea kuimarishwa ili kuhakikisha kinatoa huduma mbalimbali ikiwemo ushauri wa kisheria na msaada katika upatikanaji wa haki kwa wananchi wote.Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Zuberi Homera, amezindua rasmi programu ya “Sema na Waziri” leo Machi 17, 2026 jijini Dodoma, ikiwa ni hatua mpya ya kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za kisheria nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Homera amesema kuwa programu hiyo inalenga kuwapa Watanzania fursa ya kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja kwa Waziri na kupatiwa ufafanuzi wa haraka kuhusu masuala ya kisheria yanayowakabili.

Uzinduzi huo uliambatana na tukio la Waziri kupokea simu za moja kwa moja kutoka kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini, akisikiliza kero zao na kuzitolea majibu papo hapo.

Amesema kuwa huduma ya “Sema na Waziri” inatarajiwa kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi kwa kuwawezesha kufikisha malalamiko yao kwa urahisi zaidi na kuyapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Aidha, imeelezwa kuwa programu hiyo itaongeza ufanisi katika utatuzi wa migogoro ya kisheria na kuonesha namna Serikali inavyojali na kusikiliza wananchi wake.

 “Uzinduzi wa programu hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akihimiza viongozi wa umma kusikiliza wananchi na kuhakikisha wanapata haki zao kwa wakati.”amesema Dkt.Homera

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amesema kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ilianzisha Kituo cha Huduma kwa Mteja mwaka 2024 kama sehemu ya kuboresha huduma, na kwamba uzinduzi wa “Sema na Waziri” ni mwendelezo wa juhudi hizo za kuimarisha upatikanaji wa haki kwa Watanzania.

Amebainisha kuwa hadi sasa jumla ya malalamiko 2023 yamepokelewa, ambapo kati ya hayo, 1394 tayari yamepatiwa ufumbuzi huku mengine yakiendelea kufanyiwa kazi ili kupata suluhisho la kudumu.

Katika moja ya simu zilizopokelewa, mwananchi kutoka Geita aliuliza kuhusu lini mchakato wa Katiba mpya utakamilika. Akijibu swali hilo, Waziri Homera alisema:

“Mchakato wa Katiba ni wa wananchi na ni sehemu ya Ilani ya CCM. Kwa sasa tunasubiri hatua zinazoendelea chini ya Rais, hivyo ni vyema kuwa na subira kwani jambo hili halijaachwa.”

Kwa ujumla, uzinduzi wa programu ya “Sema na Waziri” unaashiria hatua muhimu katika kuimarisha utawala bora, uwazi, na upatikanaji wa haki kwa wananchi wote nchini.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Zainabu Katimba, amesema kuwa uzinduzi wa programu ya “Sema na Waziri” ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliyelitaka Serikali kutumia mifumo ya TEHAMA ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Katimba ameeleza kuwa matumizi ya teknolojia yatawezesha wananchi wengi zaidi kufikia huduma za kisheria kwa urahisi, bila kulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.

 “kupitia programu ya “Sema na Waziri”, wananchi watapata fursa ya kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja na kupatiwa majibu pamoja na ushauri wa kisheria kwa wakati, jambo litakalosaidia kupunguza migogoro na kuongeza uelewa wa sheria katika jamii.”amesema Mhe.Katiba

Aidha, amebainisha kuwa kituo cha huduma kwa mteja cha Wizara ya Katiba na Sheria kitaendelea kuimarishwa ili kuhakikisha kinatoa huduma mbalimbali ikiwemo ushauri wa kisheria na msaada katika upatikanaji wa haki kwa wananchi wote.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages