LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 17, 2026

YAHYA MSANGI: CHADEMA MNAJIFEDHEHESHA KIMATAIFA

Anaandika Yahya Msangi 

Nimeisoma barua ya CHADEMA waliyomwandikia Katibu Mkuu wa UN. Licha ya kurejea taarifa za uongo kama makaburi ya halaiki na watu kuchomwa viwandani wameongeza upuuzi ambao ki protokali wanajipiga kisu mgongoni.


Ukichukulia hakuna ushahidi walioambatanisha kuhusu makaburi ya halaiki wala majina ya viwanda vilivyotumika kuchoma watu utajua kuwa barua yao haitafika mbali. Wataombwa ushahidi ambao hawanao. Wamenukuu tu porojo za Larry Madowo. 


Lakini kosa kubwa la CHADEMA kwenye barua yao ni hili;


Ukimuandikia unayetaka akusaidie epuka kumkosoa. It's just simple logic. 


Katika barua yao wanadai hawana imani na aliyetumwa kuongea na wadaiwa ikiwemo Serikali. Basis ya hoja yao ni kwamba aliyetumwa ana ukaribu na Balozi Dk. Asha Rose Migiro! Eti alipokuwa UN kama msaidizi wa Ban Ki Moon walifahamiana! What a stupid accusation? 


Mtu kufanya kazi pamoja na mtu haifanyi awe hafai kupewa kazi. Migiro alikuwa msaidizi wa Katibu Mkuu. Bado wako watumishi wengi UN waliofanya kazi na Migiro! CHADEMA wanataka mtu gani kutoka UN ambaye hatakuwa anafahamiana na Migiro? 


CHADEMA wanataka kusema Katibu Mkuu wa UN alifanya kosa kumteua huyo aliyekuja? Yaani unamuomba akusaidie na hapohapo unamtuhumu kufanya kosa? Atateua yupi ambaye hakuwa chini ya Migiro?


Sawa umwambie babaako kuwa alifanya kosa kumwambia mamaako akague madaftari yako unataka ateue mwingine. 


Tukio la pili ambalo CHADEMA imejibua nguo ni taarifa waliyowasilisha kwenye Tume ya Haki za Binadamu Jijini Geneva wakishirikiana na Amnesty International. 


Tarehe 12 March kulikuwa na kikao cha UN Human Rights Council Jijini Geneva. Washiriki walitoka nchi wanachama UN, NGOs, International Organization, n.k. 


Waliowasilisha report walikuwa Oryem Nyeko kutoka Africa Human Rights Watch, Tito Magoti (mwanachadema mkereketwa) na Sikula Oniala kutoka Amnesty International. 


Baada ya kuwasilisha ukaanza mjadala. Wajumbe wengi wakahoji uhalali wa report hiyo haswa ikizingatiwa wahusika walihoji upande mmoja tu! Hakuna kokote walihoji serikali ya Tanzania! Pia wajumbe wakahoji uwepo wa ushahidi makaburi ya halaiki na viwanda vilivyochomewa maiti? 


Tito na wenzake walipoulizwa kama katika uchunguzi wao waliona kwa macho yao wenyewe makaburi ya halaiki na viwanda vilivyochomewa maiti? Wakajibu "walipewa tu taarifa". 


Watu wakajiuliza walihofu nini kutafuta maoni ya serikali? Je, waliomba kuonana na serikali wakakataliwa? Wanaweza kutoa ushahidi kuwa waliomba na walikataliwa? Wakashindwa kutoa ushahidi. 


Hatimaye kikao kiliamua kuwa report ina mapungufu makubwa kiasi kwamba haina uhalali wa kufanyiwa kazi. 


Katika kuhitimisha taarifa yao kina Tito wakakiri mapungufu na kuahidi kuyafanyia kazi. 


Mimi nilijua hawataweza kurekebisha hayo mapungufu kwa kuwa hakuna makaburi ya halaiki wala viwanda vilivyochomewa miwili ya watu. Nikajua hiyo imeishia hapo. 


Sasa inashangaza CHADEMA wamemwandikia KM wa UN kana kwamba hawana habari ya yaliyojiri kikao cha Geneva! Hivi hawajui vikao vya Geneva vinawajibika kwa Mkuu wa UN ? 


Alisoma taarifa ya kikao cha Geneva halafu asome barua ya CHADEMA si atairarua na kuitupa kwenye pipa la taka?


CHADEMA mambo ya uchaguzi yameisha! Jiandaeni kwa uchaguzi mkuu wa 2030 unless nao mtazira? 


UN ni shirika lenye mambo mazito kama vita ya Iran, Gaza, n.k. Barua yenu Haina uzito UN.



No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages