Baadhi ya jamii ya Wamasai wanaoishi, Nungwe, Mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar wameahidi kuwapigia kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kulinda amani na utulivu wa nchi pamoja na kudumisha Muungano lakini pia na kuleta maendeleo.
Wamasai hao wametoa pongezi hizo na kuahidi kuwapigia kura katika uchaguzi Mkuu ujao, waliposhiriki katika kampeni za CCM eneo la Nungwi, Kaskazini Unguja, Zanzibar Septemba 18, 2025.
Wamesema kuwa Muungano umewafanya waishi Zanzibar bila kubughudhiwa hivyo hawana kingine cha kuwapa viongozi hao zaidi ya kuwapigia kura ili waendelee kuishi kwa amani.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇