CCM Blog, Ubungo, Dar es Salaam
Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Shirika la Viwango Tanzania limefanikiwa kuandaa viwango 2,765 vya sekta mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji ya soko ambavyo vitasaidia wafanyabiashara, wajasiriamali na watoa huduma kuzalisha bidhaa bora zenye kukidhi matakwa ya viwango, hivyo kuwawezesha kufanya biashara ndani na nje ya nchi, hatua ambayo imeelezwa kuwa italeta tija na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Pia katika kipindi hicho, jumla ya vyeti na leseni za ubora 3,184 vimetolewa kwa wazalishaji, miongoni mwao wakiwemo wajasiriamali wadogo 1,359.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dk. Ashura Katunzi, akitaja mafanikio ya Shirika hilo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia, wakati wa Kikaokazi baina ya Uongozi wa TBS na Wahariri na Waandishi wa habari kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo Septemba 18, 2025, kwa uratibu wa Ofisi ya Msajli wa Hazina.
Amesema, serikali kupitia TBS imekuwa ikitenga zaidi ya sh. milioni 350 kila mwaka kwa madhumuni ya kuhudumia wajasiriamali wadogo bila ya malipo yoyote.
Dk. Ashura amebainisha kuwa leseni hizo zimesaidia wazalishaji kuweza kuzalisha bidhaa bora, ikiwa ni pamoja na bidhaa zao kuweza kuaminika sokoni na pia kufanya biashara nje ya mipaka ya Tanzania, hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Amesema, Shirika limeendelea na huduma za usajili wa bidhaa za vyakula, vipodozi na maeneo ya uzalishaji, uuzaji, usambazaji na uhifadhi wa bidhaa hizo kwa lengo la kuhakiki ubora na usalama wa maeneo hayo ili kuendelea kulinda afya za walaji ambapo jumla ya bidhaa 8,199 zilisajiliwa na maeneo 47,886 yalisajiliwa.
Akieleza uwezo wa TBS kimaabara, amesema, Maabara za TBS zina mashine za kisasa (state-of -art-equipment) zinazowezesha kupata majibu sahihi na kwa wakati na kwamba Serikali imetumia kiasi kisichopungua Sh. Bilioni 12.9 kuhakikisha mashine hizo zinapatikana.
Katika kikaokazi hicho Dk. Ashura ameeleza mafanikio lukuki ikiwa ni pamoja na mashine nyingi zilizopo katika maabara za TBS na kuzitaja moja baada ya nyingine ambazo utazisoma katika taarifa kamili baada ya maelezo ya picha hapo chini.







No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇