Jun 26, 2025

DKT. TULIA AWASHUKURU WABUNGE, WADAU KUCHANGIA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA WAVULANA BUNGE

 


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akisogeza kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la msingi kuanza ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Bunge eneo la Kikombo nje kidogo ya Jiji la Dodoma Juni 26, 2025. 

Ujenzi wa shule hiyo ya kisasa utagharimu zaidi ya sh. bilioni 3.Sehemu ya fedha hizo zimechangwa na wabunge pamoja na wadau mbalimbali nchini.

Pamoja na kuwashukuru wabunge na wadau waliotoa mchango huo, Dkt.Tulia amewahimiza wananchi, Taasisi binafsi, mashirika ya umma na wadau wa maendeleo kujitokeza kwa wingi kuunga mkono ujenzi wa shule hiyo kama sehemu ya jukumu la pamoja la kuimarisha elimu nchini.

Dkt. Tulia akisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye jiwe hilo la msingi.

Spika Dkt.Tulia akizungumza wakati wa hafla hiyo.



Baadhi ya wabunge na wageni waalikwa 

Wakiwa katika picha ya pamoja.

Spika Dkt. Tulia akimfunga vifungo mtoto aliyekwenda na wazazi wake walio jirani eneo hilo kushuhudia uwekaji jiwe la msingi.
Spika Dkt. Tulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanakijiji waliofika katika hafla hiyo.
 

Sehemu ya kiwanja patakapo jengwa shule hiyo.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages