LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 8, 2025

WANANCHI WAMIMINIKA BANDA LA LATRA-CCC 88 DODOMA KUJUA HAKI ZAO WANAPOSAFIRI

 Wanafunzi na wananchi wengine wakipata elimu kuhusu Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA-CCC), walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.


Wananchi waliofika hapo waliambiwa kwamba mtumiaji wa huduma za Usafiri Ardhini ni abiria anayesafiri kwenye basi la masafa marefu, basi la mijini (daladala),Taxi, Taxi Mtandao, Pikipiki za magurudumu mawili au matatu, pamoja na treni za abiria.


 Baraza hilo limeundwa kisheria ambapo walisema abiria  awapo safarini ana haki zifuatazo; Usalama,kupata mahitaji muhimu, kupewa taarifa awapo safarini,kuchagua,kusikilizwa,kulipwa fidia, kusafirii katika mazingira salama, kuelimishwa na haki ya kugomea huduma au bidhaa zisizokidhi viwango.







Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Miuji B, wakisikiliza maelezo






IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages