May 7, 2025

WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA MSUYA AMEFARIKI DUNIA, LEO

Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Cleopa David Msuya amefariki dunia hii leo Mei 7, 2025.

 Akitangaza, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema kifo hicho kimetikea katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam alipokuwa (Msuya) amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Rais amesema, taarifa zaidi ya Mipango kamili ya msiba itaendelea kutolewa na Serikali na ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo tarehe 7 hadi 13 Mei, 2025.

Rais Dkt. Samia amewapa pole Ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa msiba huu. jijini Dar es Salaam.

Msuya aliwahi kushika wadhifa wa Waziri Mkuu mara mbili, Mara ya kwanza ni kuanzia tarehe 7 Novemba, 1980 hadi tarehe 24 Februari, 1983, Mara ya pili ilikuwa ni tarehe 5 Desemba, 1994 hadi tarehe 28 Novemba, 1995 huku akishika pia wadhifa wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baada ya kustaafu siasa aliendelea kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika Taasisi mbalimbali za Jamii.
Cleopa Msuya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya mara baada ya kufungua mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe kwenye hafla iliyofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 09 Machi, 2025. Mzee Msuya pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mwanga.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages