Ruaha, Iringa, leo Oktoba 2, 2024
Mkoa wa Iringa umesema kutokana na juhudi kubwa za Rais wa Awamu ya Sita Dk.Samia Suluhu Hassan kubeba agenda ya kuinua sekta ya utalii kwa kutangaza kwenye mataifa mablimbali duniani vivutio vilivyopo nchini, katika kipindi cha miaka kumi kumekuwa na ongezeko la watalii katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha kutoka wastani wa watalii 5,320 mwaka 2001/2002 hadi kufikia watalii 19, 332 mwaka 2023/2024.
Hayo yamesema leo Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Maulid Surumbu na wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, mkoani Iringa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Peter Serukamba, leo Oktoba 2, 2024.
Amesema, wakati amesema, Rais Dk. Samia alipoingia madarakani kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuifungua nchi ikiwemo kuhakikisha sekta ya utalii inafahamika duniani kote kutokana na filamu yake ya "Tanzania Royal Tour" ambayo imkuwa kivutio kikubwa kwa mataifa ambayo yamehamasika kuja kutembelea hifadhi na kuwekeza hapa nchini.
"Ndugu washiriki,mafanikio haya yanatokana na juhudi za Rais Samia za kutangaza hfadhi na kuboresha miundombinu ya Barabara ,kuongeza malazi ya wageni, kuongeza mazao mapya ya utalii, kuongeza Mawasiliano ya simu na internet, kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato, kuongeza idadi ya watumishi pamoja na kuwapa Mafunzo ya idadi ya mafunzo mara kwa mara" amesema Surumbu.
Sanjari na hayo Surumbu amesema, matukio ya ujangili yamepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na hifadhi kuwa karibu na jamii kupitia mpango wa ujirani mwema pia kuishirikisha jamii kumeleta matokeo chanya hasa katika kuboresha mahusiano na kusaidia katika kutoa taarifa za uharifu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama Hifadhi ya Taifa Ruaha Regius Komba akizungumza katika Kongamano la Miaka 60 ya Hifadhi hiyo, leo.
Chifu wa Wahehe Adam Mkwawa II, akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Godwell Ole Meng'ataki wakati wa Kongamano la Miaka 60 ya Hifadhi hiyo, leo. Chifu wa Wahehe Adam Mkwawa II, akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka 60 ya Hifadhi hiyo, leo.Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama Hifadhi ya Taifa Ruaha Regius Komba akiwa na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo la Miaka 60 ya Hifadhi hiyo, leo.Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Godwell Ole Meng'ataki akiwa na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo la Miaka 60 ya Hifadhi hiyo, leo.Waanzilishi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha wakiwa kwenye kongamano hilo.
Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Maulid Surumbu (katikati, waliketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wanaoshiriki kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇