Mar 17, 2025

COSTECH YAPIGA HATUA KUBWA AWAMU YA RAIS SAMIA

 Serikali imewekeza shilingi bilioni 25.7 katika utafiti, ubunifu na maendeleo ya teknolojia kupitia Tume ya Taifa ya  Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Mafanikio hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Tume hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 17, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.

Amesema Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (2021-2025), Tanzania imeendelea kupiga hatua katika maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu. Kwa utashi thabiti wa kisiasa na dira ya kuifanya Tanzania kuwa taifa linalojegwa kwa kutumia sayansi na teknologia

 â€śHatua hii si tu kwamba imeendelea kuimarisha msingi wa maendeleo ya kisayansi, bali pia imethibitisha dhamira ya serikali ya kujenga taifa linalowekeza katika kuibua teknolojia, likiongozwa na tafiti na ubunifu.”Amesema Dkt. Nungu.

Aidha, Serikali kupitia COSTECH, imefadhili zaidi ya tafiti 50 katika sekta za Elimu, kilimo, afya, na mazingira ili kuhakikisha maarifa haya yanatumika kuboresha maisha ya Watanzania.

 Ameendelea kueleza kuwa  zaidi ya vituo vya ubunifu 111 zimeimarishwa, huku tafiti zikibadilika kuwa suluhisho za kisayansi kwa jamii. Kampuni mpya zipatazo 70 zimesajiliwa ikiwa na matokea ya wabunifu waliyowezeshwa na serikali.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Tume hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 17, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages