Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba amesema juhudi ya serikali ni kuendelea kupanua wigo wa ulinzi wa jamii, huku ikiboresha ufanisi wa programu zilizopo, na kuunganisha masuluhisho ya kidijitali ambayo ni muhimu katika kufikia idadi ya watu inayolengwa na muhimu kwa ajili ya kuunda mfumo wa ulinzi wa kijamii unaolingana zaidi na ustahimilivu.
Amesema, pia serikali itaendeleza na kudumisha kasi ya kusaidia kaya maskini na zilizo katika mazingira magumu ili kuboresha maisha yao na kupunguza umaskini kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 na Dira ya Zanzibar 2050, na kwamba Serikali imependekeza kuendelea kwa Miradi wenye tija kwa Jamii.
.
Waziri Dk. Nchemba amesema hayo wakati wa mjadala maalumu kuhusu mstakabali wa ulinzi wa jamii katika kupunguza umasikini nchini, uliofanyika katika Ukumbi Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam, leo Disemba 5, 2024 na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo.
"Serikali ya Tanzania chini ya usimamizi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akisimama mbele, itaendelea kushirikiana na marafiki na washirika wa maendeleo hivyo natoa mwito kwa uungaji mkono wa kusimamia dhamira thabiti ya rasilimali ya PSSN III katika kuboresha na kuendeleza maisha ya watu maskini na watu wanaoishi katika mazingira magumu." akasema Dk. Nchemba.
Dk. Nchemba akasisitiza kuwa Serikali ya Tanzania imethamiria kuwa na programu ambazo zitasimamia usalama wa jamii ambayo inakabiliana na umaskini na program ambazo zimeundwa kwa maono yaliyobuniwa yenye uwiano, endelevu, shirikishi na kwa Maendeleo ya watu.
Alitaja mifuko iliyoanzishwa kuwa ni Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mwaka 2000 ambao unatekeleza programu za nchi nzima za usalama wa jamii kupitia Miradi ya Mtandao yenye Tija kwa Jamii na kuanzishwa kwa Sera ya Kitaifa ya Hifadhi ya Jamii ya 2023 na kwamba pamoja na mambo mengine, imewezesha Tanzania kupunguza umaskini uliokithiri kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011 hadi 26.4% mwaka 2018.
Dk. Nchemba alisema kutokana na hali hiyo serikali inatatarjia idadi ya watu masikini itabadilika kwa kiasi kikubwa, kwani serikali imeanza maandalizi ya Utafiti wa Kaya masikini katika Bajeti yake ya 2024-25.
Akifunga Mjadala huo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Menejiment Utumishi wa Umma, Ridhiwani Kikwete amesema, mjadala huo wa leo ulete maendeleo katika kupunguza umasikini katika kaya hapa nchini.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Shedrack Mziray amesema mpango wa kunusuru kaya masikini unahudumia kaya milioni moja na laki tatu,(1,300,000) lakini tathmini imefanyika kuona kaya ambazo zimeboreka kimaisha ni laki nne (400,000) ambazo watahitimisha kuzihudumia katika mpango huo wa kunusuru kaya masikini.
"Mpango umefanikiwa, tuliwapa taarifa kaya takribani laki nne kuwaondoa kwenye mpango huo kutokana na kuona kuwa sio masikini sana, kwa hiyo tunapokwenda kwenye mwaka mmoja wa kukamilisha tumebakiwa na kaya takribani laki tisa na nusu ambazo tutaendelea nazo." Mziray akasema.
Pamoja na mafanikio hayo Mziray ameeleza kuwa changamoto ambayo wanakumbana nayo ni kaya masikini kutojiondoa katika mpango huo wa kunusuru kaya masikini licha ya kwamba kwa sasa TASAF kwa kushirikiana na Serikali imetengeneza sheria ya kuwaondoa katika mpango huo kaya nufaika kwa miaka mitatu mitatu ingawa kuna baadhi ya kaya kama za wazee na watu wenye ulemavu huendelea kubakia kutokana na hali zao.
Kwa upande wake, Wazir wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Saada Mkuya amesema pia wao ni wanufaika wa mpango huo wa TASAF wa kunusuru kaya masikini kwa kujengewa skuli na kuwapatia kila kaya sh.14,000 kwa kila mwenzi na pia kuwapeleka watoto shule na kuwapatia huduma za afya bila masharti huku wengine wakipewa mitaji ya kufuga kuku.
Pia amesema TASAF imewapatia wakulima msada wa kujenga matuta makubwa ili maji yasiingie kwenye mashamba ya mazao yao na kwamba imewasaidia sana kuweza kupata mazao mengi zaidi.
Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa mjadala wa mstakabali wa ulinzi wa jamii katika kupunguza umasikini nchini, uliofanyika katika Ukumbi Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam, leo Disemba 5, 2024.
Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa mjadala wa mstakabali wa ulinzi wa jamii katika kupunguza umasikini nchini, uliofanyika katika Ukumbi Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam, leo Disemba 5, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Saada Mkuya akizungumza wakati wa mjadala wa mstakabali wa ulinzi wa jamii katika kupunguza umasikini nchini, uliofanyika katika Ukumbi Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam, leo Disemba 5, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Jakaya Kikwete, akifurahia jambo wakati akizungumza wakati wa mjadala wa mstakabali wa ulinzi wa jamii katika kupunguza umasikini nchini, uliofanyika katika Ukumbi Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam, leo Disemba 5, 2024.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Nadhan Belete, akizungumza wakati wa mjadala wa mstakabali wa ulinzi wa jamii katika kupunguza umasikini nchini, uliofanyika katika Ukumbi Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam, leo Disemba 5, 2024.
Washiriki wakiwa kwenye mjadala huo.
Washiriki wakiwa kwenye mjadala huo.Washiriki wakiwa kwenye mjadala huo.Washiriki wakiwa kwenye mjadala huo.Washiriki wakiwa kwenye mjadala huo.Washiriki wakiwa kwenye mjadala huo.Meza kuu wakiwa kwenye mdahalo huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha Benny Mwaipaja, akiongoza uratibu wa mjadala huo.
Picha za kumbukumbu Dk. Nchemba na washiriki wa mjadala huo.👇👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇