LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 21, 2024

HEKAHEKA KLINIKI YA ARDHI KINONDONI ZAPAMBA MOTO

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog

LEO Disemba 21, 2024 ikiwa siku ya tano tangu Huduma ya Kliniki ya Ardhi ilipoanza Disemba 16, 2024, hekeheka za wananchi kupata huduma hiyo zimepamba moto leo, kila mmoja akijitahidi ili aondoke na hati.


Huduma hiyo inafanywa mahsusi kukamilisha kazi ya urasimishaji ardhi ambao mchakato wake ulianza tangu wakati wa uongozi wa serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dk. john Magufuli ambaye sasa ni hayati.


Miongoni mwa changamoto zinazojitokekeza ni baadhi ya maofisa kwenye Kliniki hiyo kutoa maelekezo yanayokinzana kutoka mmoja hadi mwingine. Mmoja akitoa utaratibu wa kufuatwa na wateja baada ya muda mwingine anatoa utaratibu tofauti.


Hadi kufikia leo wapo ambao walishalipia fedha ili kupatiwa hati lakini hadi leo walikuwa hawajapata.


Changamoto nyingine, ni kwa wale ambao wanalazimika kufuata mtiririko mpya wa kujaza fomu za taarifa zao na kisha kufunguliwa faili jingine, licha ya kwamba mafaili yao yalishafika miezi kadhaa nyuma Ofisi ya Ardhi ya Manispaa kwa ajili ya hatua mbalimbali.


Miongoni mwao wapo ambao walikuwa wameshalipia ada ya awali na walikuwa walisubiri control number kwa ajili ya kulipia ada rasmi ya kupatuwa hati.


Hata hivyo baadhi ya wananchi wamesifu juhudi za kuanzishwa kliniki hiyo na kuomba ziongezwe siku ili wale ambao watakuwa hawajapata huduma hiyo waipate.


Huduma hiyo amvayo inafanyika eneo la Interchick, katika viwanja vya majengo ya Hospitali ia IMTU inaelezwa kuwa inafungwa kesho.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages