KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk
Emmanuel John Nchimbi, ameongoza maelfu ya waombolezaji wakiwemo
viongozi na wananchi kutoka maeneo mnalimbali nchini, walioshiriki
mazishi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, marehemu
Tixon Nzunda, yaliyofanyika huko Msinde, Kata ya Mpemba, Wilaya ya
Mbozi, mkoani Songwe, Jumamosi Juni 22, 2024.
Marehemu Nzunda, ambaye hadi mauti yanamkuta kwa ajali ya gari Juni 18, 2024, akiwa ziara ya kikazi wilayani Hai, alikuwa mtumishi mwandamizi wa Serikali, akiwa amewahi kutumikia nafasi mbalimbali za utumishi wa umma, ikiwemo kuwa katibu mkuu wa wizara mbalimbali, baada ya kupanda ngazi za utumishi wa umma kutokea kuwa Ofisa wa Serikali ngazi ya wilaya.




No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇