LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 23, 2024

WAJUMBE HALMASHAURI KUU CCM WILAYA YA KIBAHA MJINI KUKUTANA SAA SABA LEO

Na Dismas Lyassa, Kibaha

Huku uchaguzi wa Serikali za mitaa ukionekana kukaribia, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mjini leo saa saba mchana wanakutana ili kujadili mambo mbalimnbali ya maendeleo na mikakati ya chama hicho.

Kulingana na taarifa ya Katibu wa CCM Wilaya Kibaha mjini Ndg Issack R.Kalleiya kikao hicho kitafanyika ukumbi wa CCM Wilaya Kibaha.

"Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Ndg Issack R.Kalleiya anapenda kuwakaribisha /kualika wajumbe wote wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya Kibaha mjini kutakuwa na kikao cha halmashauri kuu CCM Wilaya Kibaha mjini  leo  siku ya Jumapili tarehe ya 23/06/2024, saa Saba kamili mchana. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI," inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Wana CCM katika kata na matawi mbalimbali wanakipongeza Chama cha Mapinduzi kutokana na uimara wake na ushirikiano mzuri wa viongozi wa juu chini ya mwenyekiti wake Mwl Mwajuma Nyamka na katibu  Issack R.Kalleiya.

"Mwl Nyamka amekuwa zaidi ya mwalimu sasa, ni mwenye busara na hekima mno, chama kinakwenda vizuri mno Kibaha Mjini. Ndugu yetu Issack R.Kalleiya tangu amekuja Kibaha mjini amekuwa bega kwa bega na sisi wana CCM, ofisi yake ni yetu, kwa kweli tunakwenda vizuri," anasema mzee mmoja mwana CCM maarufu ambaye hakupenda jina lake liandikwe akisisitiza kuwa ombi kuu kwa wana CCM ni kuhakikisha hakuna hata mtaa mmoja unachukuliwa na upinzani. 

Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini ndugu Issack R.Kalleiya.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages