Na Dismas Lyassa, Kibaha
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha mjini ndugu Silvestry Koka katika kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo ametoa mifuko 100 ya sarufi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kuishi katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha mji.
Koka ametoa hilo wakati wa kikao cha baraza kuu UWT Wilaya ya Kibaha ambacho kilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama pamoja na jumuiya za chama.
Koka alibainisha kwamba lengo lake kubwa ni kushirikiana bega kwa bega na jumuiya zote za chama ili kuweza kuweka mipango ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
“Mimi kama Mbunge wa Jimbo hili kwanza nawashukuru sana wanawake wa UWT, kwa kuweza kunialika katika baraza hili na nimeguswa na mimi katika ujenzi wa nyumba ya mtumishi nitachangia mifuko 100 ya saruji,”alisema Mbunge Koka ambaye amekuwa msaada wa masuala mengi ya maendeleo ya chama katika jimbo.
Mbunge huyo ambaye amekuwa akishiriki ujenzi wa ofisi nyingi za chama pamoja na maendeleo mengine ya kukiimarisha chama, aliwahimiza wanawaje hao kuendelea kumpa ushirikiano wa hali na mali katika kutekeleza shughuli mbali mbali za kimaendeleo na kuwatumikia wananchi.
Koka alisema pia wanawake hao wanapaswa kuwa na mshikamano kuamzia katika ngazi za chini na kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili kuweza kushinda kwa kishindo.
Mngoja alifafanua kwamba pamoja na kumshukuru Mbunge amewashukuru baadhi ya wabunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuchangia misaada mbali mbali ya ujenzi wa nyumba hiyo ya mtumishi.
Katika hatua nyingine Mngoja alisema kwamba walifanya harambee kwa ajili ya ujenzi huo ambapo wamefanikiwa kupata matofali zaidi ya 2500, pamoja na mifuko ya saruji.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka amewataka wanawake kujikita zaidi ya kushinda katika chaguzi mbali mbali.
“Jukumu la UWT ni kushinda katika chaguzi mbali mbali ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025,”alisema Nyamka.
Kikao cha baraza kuu la umoja wa wanawake wa (UWT) kimekutana na kujadili mambo mbali mbali ikiwemo kupatiwa mafunzo ya utunzaji wa fedha pamoja na umuhimu ya kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇