LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 23, 2024

CCM KIBAHA MJINI YALAANI MAUAJI YA ASIMWE, KATIBU CCM TAWI LA MISWE CHINI

 

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwl Mwajumla Nyamka akiongea jambo, huku kulia Mbunge wa Jimbo hilo ndugu Silyvestry Koka akitafakari jambo. 

Na Dismas Lyassa, Kibaha Mjini

CHAMA Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mjini Mkoani Pwani kimelaani mauaji ya madereva wa bodaboda (almaarufu Maafisa Usafiri).

Kulingana na taarifa iliyolewa leo Jumapili Juni 2024, mojawapo ya mauaji ni yale yaliyotokea kwa Katibu wa CCM Tawi la Miswe Chini, Kata ya Mbwawa, ndugu Sitakiwi Ramadhan Pazi yaliyotokea hivi karibuni.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Ndg Issack R.Kalleiya

Tamko hilo lililotolewa na Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kibaha Mjini leo, linasema CCM kinalaani mauaji ya kikatili yaliyofanywa kwa motto Asimwe Novat (mlemavu wa ngozi albino) Mkoani Kagera, mwenye umri wa miaka miwili ambaye alitoweka Mei 30 mwaka huu na kupatikana akiwa amefariki huku baadhi ya viungo vya mwili wake vikiwa vimenyofolewa.

“Tunaomba Jeshi la Polisi kuendelea kuchukua hatua stahiki ili sheria ichukue mkondo wake,”
 imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha kinatoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa hatua ambazo limeanza kuzichukua na kuwatia mbaroni baadhi ya watuhumiwa na tunaomba waongeze kasi ili hali hii itoweke kabisa nchini.



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages