Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza ametoa salamu za pole kwa waliofariki na majeruhi wa ajali iliyotokea katika Mlima Iwambi Mbalizi mkoani Mbeya Juni 7, 2025. Ametoa salamu hizo za pole wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni Dodoma Juni 9, 2025, alipokuwa akiuliza swali kwa niaba ya Mbunge wa Viti Maalumu, Suma Ikenda.
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali mbaya iliyotokea usiku wa tarehe 7 Juni 2025, mlima Iwambi Mbalizi na kusababisha vifo vya wananchi 28 na majeruhi 8."
"Natoa pole kwa wafiwa wote na naungana na familia za marehemu na wote walioguswa na msiba huu mkubwa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi."
Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape majeruhi wote nafuu ya haraka, na azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, AMEN.
Oran Manase Njeza (MB)
Mbunge Jimbo la Mbeya Vijijini
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇