Na Joctan Agustino,NJOMBE
Wachimbaji wadogo wa madini wilayani Ludewa mkoani Njombe wameiomba serikali kuwapatia vitalu katika migodi ya Makaa ya mawe na chuma iliyopo katika vijiji vya Liganga Nchuchuma ili kuongeza kufanyabiashara wanaochipukia katika sekta hiyo.
Wachimbaji hawa wadogo akiwemo Isaya Mhagama na John Hiluka wametoa ombi hilo katika ziara ya Naibu waziri wa madini Dr Steven Kiruswa wakati akikagua maandalizi ya awali ya kuanza machimbo ya mkaa wa mawe katika kijiji cha Ketewaka kilichopo tarafa ya Masasi wilayani Ludeewa.
Licha ya wawekezaji wadogo katika sekta ya madini kuiweka bayana pendekezo lao kabla ya kuanza uchimbaji katika kigodi hiyo , mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph kamonga na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Sanday Deogratus wamewatoa hofu juu ya takwa lao na kisha kuendelea kutoa hamasa kununua vitalu katika maeneo yenye hazina ya madini
Serikali inakusudia mwezi September kulipa fidia kiasi cha zaidi ya bil 16 kwa watu walipisha miradi ya Liganga na Nchuchuma ili kuanza rasmi mchakato wa machimbo hayo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇