Kingjada Hotel. Dar es Salaam
Mfuko wa 'Small Entrepreneurs Loan Facility (SELF) Project', umefanikiwa kuongeza upatikanaji wa huduma za mikopo kwa wananchi wa kipato cha chini (financial inclusion), ambapo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi kufikia June 30, 2025 umetoa mikopo yenye thamani ya Sh. Bilioni 196.9 huku kiwango cha mikopo chechefu kikiwa chini ya asiimia 10.
Pia Mfuko umeweza kujiendesha kwa kupata faida huku mikopo ikiwa imewafikia wanufaika wapatao 183,381, kati yao wanawake wakiwa 97,170 sawa na asilimia 53 na wanaume 86,211 sawa na asilimia 47.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa SELF Santiel Yona, katika kikaokazi baina ya Mfuko na Wahariri na Waandshi wa habari, kilichofanyika leo Agosti 15, 2025 jijini Dar es Salaam, kikisimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, iliyokiratibu kwa lengo la kuimarisha uelewa wa Wahariri hao kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko.
Mtendaji Mkuu huyo amesema pia Mfuko umefanikiwa kukopesha na kujenga uwezo wa taasisi za huduma ndogo za fedha (MFIs) kutoka mwaka 2021 akifafanua kuwa hadi kufikia Juni 30, 2025, Mfuko umezikopesha na kuzijengea uwezo taasisi 549 za huduma ndogo za fedha.
"Kuzijengea uwezo wa taasisi hizi katika masuala ya huduma ndogo za fedha kunasaidia kupunguza changamoto za uendesahaji wake lakini pia kutengeneza ajira kwa kuwa Mfuko wa SELF umesaidia kutengeneza ajira kwa wakopaji wao wenyewe na wale wanaowaajiri, kiasi cha ajira 183,381 kimetengenezwa kutoka mwaka 2021 –June 2025", amesema Mtendaji Mkuu huyo.
Amesema, katika kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika kapeni yake ya nishati safi ya kupikia, SELF imeanza kutoa mikopo kwa ajili ya nishati hiyo kwa ajili ya upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ambapo pamoja na mikopo kwa ajili hiyo pia Mwaka 2021-June 2025 Mfuko uliweza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wapatao 10,378.
Mtendaji Mkuu huyo (pichani) amezungumza mengi muhimu katika kikao kazi hicho, ili uweze kuyapata vizuri, baada ya picha yake, tumekuwekea wasilisho lote kama alivyoliwasilisha.
Your Ad Spot
Aug 15, 2025
Home
featured
Uchumi
SELF YATOA MIKOPO YA SH. BILIONI 196.9 KWA WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI, YAMSHUKURU RAIS DK. SAMIA KWA KUIIMARISHA
SELF YATOA MIKOPO YA SH. BILIONI 196.9 KWA WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI, YAMSHUKURU RAIS DK. SAMIA KWA KUIIMARISHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot






















No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇