Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Bara Christina Mndeme amewasili jijini Luanda nchini Angola kumwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Daniel Godfrey Chongolo na kupokelewa na Katibu Mkuu wa MPLA Paulo Pombolo.
Akiwasilisha salamu za CCM Ndg. Mndeme amewashukuru sana wanachama na viongozi wote wa chama cha MPLA kwa kuendelea kudumisha amani katika nchi hiyo .
Amewahakikishia wanachama wa MPLA pamoja na wananchi wote kwamba, Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti Mahiri Ndg. Samia Suluhu Hassan ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatakia Uchaguzi mwema ambapo, wananchi wa Angola wanatarajia kupiga Kura na kumchagua Rais pamoja na Wabunge Kesho tarehe 24 Agosti 2022 Nchini Angola.
Ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake nchini humo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Bara Ndg. Christina Mndeme ameshiriki mkutano wa kufunga Kampeni za Uchaguzi wa Chama Tawala Cha MPLA uliofanyika katika mji wa Camama Jijini Luanda nchini Angola.
Sambamba na kushiriki Ndg. Mndeme amewasihi wana Angola kudumisha Amani katika kipindi hiki cha kuhitimisha Kampeni na baada ya matokeo ya uchaguzi katika Nchi hiyo.
Aidha, katika Mkutano huo, Mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama Cha (MPLA) ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi wa Angola Sera na mipango ya chama chake hususani kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta mbalimbali, endapo atachaguliwa tena kuwa Rais wa nchi hiyo, amewaomba wananchi wa Angola kukipigia kura chama cha (MPLA) kwa maendeleo ya kweli katika nchi ya Angola.
Vyama vya Siasa Nane (8) vinatarajiwa kushiriki katika Uchaguzi huo, kikiwemo Chama Cha MPLA .
Katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Bara ameongozana na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Organaizesheni CCM Taifa Ndg. Solomon Itunda.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇