Naibu katibu Mkuu wa CCM Ndg. Christina Mndeme ameshiriki katika zoezi la uangalizi wa Uchaguzi Mkuu uliyofanyika nchini Angola leo tarehe 24/08/2022 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake nchini Angola akimwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Ndg Daniel Godfrey Chongolo.
Ndg. Mndeme ameungana na waangalizi wengine wa kimataifa kuviwakilisha vyama vya siasa.
Aidha, katika zoezi hilo Ndg. Mndeme aliongozana na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Organization CCM Taifa Ndg. Solomon Itunda.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇