LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 28, 2021

NAIBU WAZIRI NDEJEMBI AWAKABIDHI WANUFAIKA WA MKURABITA HATIMILIKI ZA KIMILA 106 KIJIJI CHA MANYEMBA,, CHAMWINO+video


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amekabidhi hati miliki za kimila 106 kwa wakulima wadogo wadogo wa miwa katika Kijiji cha Manyemba wilayani Chamwino, Dodoma.

Ndejembi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino, amewaasa wananchi wa Manyemba kuacha kusababisha migogoro kwa kuuza mashamba ambayo tayari wameyarasimisha, lakini pia amewataka kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza kijijini hapo.

Mashamba ya wakulima hao yamepimwa kwa ushirikiano wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Naibu Waziri Ndejembi akiungana na kikundi cha ngoma  kupiga ngoma huku wakicheza na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,Gift Msuya walipowasili kwenye hafla ya kukabidhi hatimiliki za kimila 106 kwa wakulima wadogo wadogo wa miwa katika Kijiji cha Manyemba.
Naibu Waziri Ndejembi ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, akimtambulisha kwa wananchi Mkuu mpy wa Wilaya ya Chamwino, Gift Msuya.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Manyemba, Habib akifungua mkutano huo.



Mratibu wa MKURABITA, CPA, Dkt. Seraphia Mgembe akielezea jinsi Mkurabita inavyofanikisha kurasimisha mali za wanyonge nchini ambapo hadi sasa imefanya kazi hiyo katika halmashauri za wilaya 60.
Ofisa wa Benki ya NMB Chamwino, Emil Mrumah akielezea umuhimu wa wananchi wa Manyemba kujiunga na benki hiyo ili wapate fursa ya kukopa kwa kutumia kama dhamana hati miliki za kimila walizokabidhiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Gift Msuya akiishukuru MKURABITA  kwa kazi nzuri ya kurasimisha  mashamba ya wakulima  pamoja na kuwapatia Hati miliki  lakini amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi fursa kama hizo zinapotokea kijijini hapo.
Naibu Waziri, Ndejembi akiwahutubia wananchi wa Manyemba na kuwaasa kutouza mashamba yaliyorasimishwa.
Ndejembi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, akikabidhi hatimiliki za kimila kwa baadhi ya wakulima waliorasimisha mashamba yao.





PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

 

Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, ujue yaiyojiri wakati wa hafla hiyo.....
 

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda

 Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 

0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages