Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema usikivu wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan ndiyo uliowezesha Serikali kuamua kuondoa zuio la mabsi kusafiri usiku na kuruhusu safari hizo na kwamba tathmini ya mwaka mmoja wa utekelezaji wa ruhusa hiyo imeonyesha kuwa wananchi wengi wamefurahishwa na kuridhishwa na maamuzi hayo ya Serikali.
Imesema kutokana na hali hiyo kuna mwitikio mkubwa wa Wananchi kutumia usafiri wa usiku kuliko mchana, na msongamano wa abiria kwenye Stendi umepungua, na ‘mchezo’ wa mabasi kukimbizana umepungua sana na unaelekea kwisha kabisa huku tathmini hiyo ya LATRA ikionesha kuwa safari hizi za usiku zimepunguza gharama za njiani kwa abiria na kuboresha matumizi ya muda wao kwenye shughuli za kiuchumi, kijamii na kujiongezea vipato.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habibu Suluoleo, wakati akitoa wasilisho la Mafanikio ya LATRA katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Dk. Samia, kuanzia Februari, 2021 hadi Machi 2025, alipokuwa katika Kikao na Wahariri wa Taasisi za Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajiri wa Hazina (OTR) ambacho kimefanyika Jijini Dar es Salaam, leo
Aprili 14, 2025.
"Serikali ya Awamu ya Sita iliondoa zuio la mabasi ya abiria kusafiri nyakati za usiku lililowekwa mwaka 1994. Akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti tarehe 28 Juni, 2023, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa aliziagiza, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Uchukuzi kuweka utaratibu mzuri wa usimamizi wa mabasi nyakati za usiku.
LATRA ilishiriki katika zoezi la kufanya maandalizi ya kuanza kwa safari za usiku kwa kushirikiana na wadau wake muhimu, hasa wamiliki wa mabasi wakiwemo TABOA na ilitekeleza maamuzi ya Serikali kwa kuanza kutoa ratiba za mabasi kusafiri usiku na mchana kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2023.
Septemba 29, 2023, akitangaza kwa niaba ya Serikali kuanza kwa ratiba za safari za usiku, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, alieleza sababu sita za Serikali kuruhusu safari za usiku", akasema CPA Suluoleo.
Akazitaja sababu hizo kuwa ni Udhibiti wa usalama kupitia Jeshi la Polisi umeimarishwa kutokana na jitihada za Serikali ya Dk. Samia, Mwamko wa wananchi, hususan wafanyabiashara kutumia taasisi za kifedha badala ya kusafiri na fedha taslimu (cash) umeongezeka na Serikali imeimarisha huduma za mawasiliano ya simu kwa kujenga minara ya mawasiliano kwenye maoneo mengi Nchini.
Sababu nyingine alizitaja kuwa ni Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inao Mfumo madhubuti wa kufuatilia Mwenendo wa Mabasi (VTS) unaofanyakazi kwa saa 24, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi imeboresha miundombinu ya usafiri, hususan barabara kuu na barabara za mikoa na hivyo kufanya Nchi yetu kuwa moja ya Nchi zenye usafiri wa barabara unaoaminika na bora, Wafanyabiashara wengi wanaomiliki mabasi ya abiria walio tayari kufanya safari za saa 24 wako tayari pia kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo kuhusu usafiri na usafirishaji wa abiria.
Apr 14, 2025
LATRA: USIKIVU WA RAIS DK. SAMIA NDIO ULIOWEZESHA SAFARI ZA MABASI USIKU
Tags
featured#
Uchumi#
Share This

About Bashir Nkoromo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇