HABARI MPYA

Your Ad Spot

Sunday, May 30, 2021

JAMII YA WAFUGAJI MBARALI WAISHUKURU MKURABITA KUWAKUMBUKA KUWAJENGEA UWEZO KIUCHUMI+video

Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Risilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu akimuelekeza jambo kwenye simu janja mmoja wa vijana wa jamii ya wafugaji, Mussa Letema wakati wa zoezi la kukusanya taarifa za dodoso kupitia mfumo wa Kobo wakati wa mafunzo ya kuwawezesha kiuchumi watu wa jamii ya wafugaji kwa kutumia hati miliki za kimila kuweka kama dhamana kukopa fedha benki za kusaidia kuboresha mifugo yao pamoja na kuanzisha miradi mingine ili kuinua kipato chao.
Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Grace Samweli akiiingiza kwenye simu janja taarifa za dodoso kwa kutumia mfumo rahisi wa ukusanyaji wa taarifa wa Kobo.

Jamii ya Kimasai akitoa taarifa sahihi kuhusu maisha kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji wa taarifa wa Kobo kwenye simu.Anayekusanya ni Afisa Mifugo, Abbasi Mubango.
Mwenyekiti wa Jamii ya wafugaji wa Kitongoji cha Mogelo, Tirike Taikoo, akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Meneja wa Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, ambao ni waratibu wa mafunzo hayo, Temu akielezea umuhimu wa jamii hiyo ya wafugaji kutumia hati miliki za kimila kukopa fedha benki.
Talasi Taikoo (kushoto) ambaye ni mmoja wa jamii hiyo aliyefanikiwa kukopa fedha benki kwa kutumiahali miliki za kimila.
Temu akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Mahusiano wa Tawi la NMB Wilaya ya Mbarali, Jones Mugyabuso akielezea umuhimu wa Jamii ya wafugaji kujiunga na benki hiyo ili wapate mikopo ya kunenepesha mifugo na kuanzisha miradi mingine ili kuinua kipato chao.
Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Grace Samwel akielezea sheria na taratibu za kuanzisha ushirika wa Jamii ya wafugaji na faida lukuki watakazopata.
Jamii ya wafugaji ambao asilimia kubwa ni wamasai wakisikiliza kwa makini wakati wataalamu wakiwafundisha.

Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Anthony Mashilindi akieleze umuhimu wa jamii hiyo ya wafugaji kupima mashamba yao ili wapate halimiliki.
Afisa Kilimo wa halmashauri hiyo, Issa Mwambela akiwafundisha  kanuni bora za kilimo ikiwemo uandaaji wa mashamba, kutumia mbolea sahihi ili kupata mavuno bora. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


 Na Richard Mwaikenda, Mbarali.

WAFUGAJI Jamii ya wafugaji (Wamasai), wameishukuru Mkurabita kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo kiuchumi yaliyofanyika katika Kijiji cha Mogelo, wilayani Mbarali, Mbeaya Mei 27, 2021.

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), yaliendeshwa na wataalamu Kilimo, Ushirika, Ardhi, Ufugaji Nyuki kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali pamoja na maofisa wa Benki kutoka CRDB na NMB.

Walifundishwa jinsi ya kutumia Hati miliki za Kimila  kuweka kama dhamana kukopa fedha benki, faida za kujiunga na Ushirika, kufuata kanuni za ufugaji wa mifugo na hasa ng'ombe, kanuni za kilimo bora cha mazao mbalimbali, kuthaminisha mali zao, kuweka vizuri kumbukumbu za mahesabu.
 
Mafunzo hayo yaliratibiwa na Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini, Anthony Temu ambaye awali aliwaeleza historia na majukumu ya  Mkurabita na kuwaeleza umuhimu wa kurasimisha ardhi zao ili wapate hatimiliki za kimila ziwasaidie kukopa fedha benki ili waanzishe miradi ikiwemo kunenepesha mifugo yao.

Mdau nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video ujue yaliyojiri wakati wa mafunzo hayo....

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

Tafadhali andika maoni yako kuhusu habari hiyo uliyosoma. Andika hapo👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages