LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 30, 2021

RAIS SAMIA ATEUA, APANGUA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

 




                

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa, kuwahamisha baadhi na wengine kuwabakisha katika vituo vyao vya kazi.

Pia amefanya uteuzi wa viongozi wakuu wa taasisi kama ifuatavyo;

Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa.

1.     Amemteua Bw. Rodrick Mpogolo kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mpogolo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara.

2.     Amemteua Dkt. Athuman Juma Kihamia kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Kihamia alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

3.     Amemteua Bw. Hassan Abbas Rugwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Rugwa alikuwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.

4.     Amemteua Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mganga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma.

5.     Amemteua Bw. Mussa Ramadhan Chogello kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huo Bw. Chogello alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais.

6.     Amemteua Bw. Ngusa Dismas Samike kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Kabla ya uteuzi huo Bw. Samike alikuwa Katibu wa Rais, Ikulu.

7.     Amemteua Mhandisi Mwanaisha Tumbo kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Pwani. Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Tumbo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.

8.     Amemteua Bi. Doroth Aidan Mwaluko kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida. Kabla ya Uteuzi huo Bi. Mwaluko alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu).

9.     Amemteua Mhe. Balozi Batilda Salha Buriani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi huo Mhe. Balozi Buriani aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya na Japan.

10.                       Amemteua Bi. Azza Hilal Hamad kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya uteuzi huo Bi. Azza aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga.

11.                       Amemteua Bi. Pili Hassan Mnyema kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga. Kabla ya uteuzi huo, Bi. Mnyema alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais.

 

Makatibu Tawala wa Mikoa waliohamishwa vituo vya kazi;

12.                       Amemhamisha Dkt. Seif Abdallah Shekillage aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.

13.                       Amemhamisha Bi Karoline Albert Mthapula aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.

14.                       Amemhamisha Bw. Albert Gabriel Msovela aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.

15.                       Amemhamisha Dkt. Angelina Mageni Lutambi aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya.

16.                       Amemhamisha Bi. Mariam Amri Mtunguja aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.

17.                       Amemhamisha Bw. Abdallah Mohamed Malela aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara.

18.                       Amemhamisha Bi. Judica Haikase Omari aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Njombe.

19.                       Amemhamisha Bw. Denis Isdory Bandisa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

20.                       Amemhamisha Bw. Missaile Albano Musa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.

 

Makatibu Tawala wa Mikoa wanaobaki katika vituo vyao vya kazi;

21.                       Bi. Happiness William Seneda anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.

22.                       Prof. Faustine Kamuzora anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

23.                       Bw. Rashid Kassim Mchatta anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma.

24.                       Bi. Rehema Seif Madenge anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi.

25.                       Bw. Steven Mashauri Ndaki anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.

26.                       Bw. Msalika Robert Makungu anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora.

Watendaji Wakuu wa Taasisi;

27.                       Amemteua Bw. William Erio kuwa Afisa Mtendaji Mkuu, Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC). Kabla ya uteuzi huo Bw. Erio alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

28.                       Amemteua Dkt. John Kedi Mduma kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mduma alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu, Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC).

 

Uteuzi huu wa Makatibu Tawala umeanza leo tarehe 29 Mei, 2021 na wataapishwa tarehe 02 Juni, 2021 saa 4:00 asubuhi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

29 Mei, 2021

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages