Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Dk. John Magufuli.
Na Debora C. Kiyuga ✍🏽
Mitano ya Magufuli, Serikali imeshughulikia kero mbalimbali za wananchi, hususan wakulima, wavuvi, wafugaji, wafanyabiashara, wafanyakazi, wajasiliamali; na bila kusahau migogoro ya ardhi.
Mitano ya Magufuli, kwa upande wa wakulima, wavuvi, wafugaji na wafanyabiashara; Serikali imefuta takriban tozo 114 zilizokuwa zikikwamisha shughuli zao.
Mitano ya Magufuli, kwa upande wa wafanyakazi Serikali ilitoa fursa ya kuajiri watumishi wapya wenye sifa wapatao 74,173 na ajira zingine bado zinaendelea. Vilevile, iliwapandisha vyeo watumishi 306,917 na kulipa madeni ya watumishi ya mishahara na yasiyo ya mishahara yenye thamani ya shilingi bilioni 472.6
Mitano ya Magufuli, Serikali imepunguza kodi ya mapato kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9 na kulipa deni la shilingi trilioni 1.2 ambapo ilikuwa ikidaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii; na hivyo kuwezesha wastaafu kuendelea kulipwa mafao yao.
Mitano ya Magufuli, kwa upande wa wajasiliamali wadogo, wakiwemo machinga, mama lishe, waendesha bodaboda na bajaji, Serikali imejitahidi kuwawekea utaratibu mzuri wa kuendesha shughuli bila ya kubughudhiwa kwa kuwapatia vitambulisho maalum vilivyotolewa kwa gharama nafuu.
Mwaka jana (2019) jumla ya wajasiliamali wadogo 1,591,085 walipatiwa vitambulisho na hivyo kuwafanya waondokane na usumbufu uliokuwepo zamani kabla ya utaratibu huo kuanza ambapo wajasiliamali wadogo walikuwa wakibugudhiwa sana na mgambo, ikiwemo kunyang’anywa mali zao.
Mitano ya Magufuli, Serikali imetunga Sheria yenye kuzitaka halmashauri zote kutenga asilimia 10 ya mapato yao kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa wanawake (asilimia 4), vijana (asilimia 4) na wenye ulemavu (asilimia 2), ambapo hadi mwezi Machi, kiasi cha shilingi bilioni 93.2 kilikuwa kimetolewa.
Mitano ya Magufuli kwa upande wa migogoro ya ardhi baadhi ya hatua ambazo serikali ilichukua ni kuanzisha Ofisi za Ardhi kwenye Mikoa yote, ambapo sasa huduma zote za upangaji, upimaji, umilikishaji, utathmini pamoja na usajili wa hati, nyaraka, ramani na michoro zinapatikana hali ambayo imeongeza kasi ya urasimishaji makazi ya wananchi na pia utoaji hati.
Mitano ya Magufuli, Jumla ya maeneo ya viwanja yaliyorasimishwa yamefika 764,158 na Serikali imetoa hatimiliki za kimila 515,474. Aidha Serikali imefanya uamuzi wa kuvirasimisha vijiji 920 kati ya 975 vilivyokuwa kwenye maeneo ya hifadhi.
#Magufulimitanotena
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇