MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Stephen Wasira amewahakikishia wananchi wa Tunduma Mkoani Songwe kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan iitahakikisha inatatua changamoto ya uhaba wa maji katika eneo hilo na Mkoa kwa ujumla.
Amesema katika kutatua changamoto ya maji Machi 20 mwaka huu Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba watakuwa Tunduma kwa ajili ya kuingia makubaliano na mkandarasi atayekajenga Mradi wa maji kwa ajili ya kutatua kero hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mji wa Tunduma Mkoani Songwe ,Wasira amesema tayari Serikali imewekq mkakati wa kumaliza changamoto ya uhaba wa maji kupitia Mradi huo ambao utaanza kutekelezwa baada ya mkandarasi kusaini mkataba wa kutekeleza ujenzi wa mradi huo.
“Nimekuja hapa kuwaambia changamoto hii ya maji ambayo ni ya muda mrefu ya uhaba wa maji inakwenda kupata ufumbuzi.Machi 20 mwaka huu mawaziri wawili wa maji na fedha watakuja kusaini mkataba na mkandarasi atakayejenga mradi huo.”
Kuhusu kero ya msongamano wa malori ,Wasira amesema atawasiliana na Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega ili kuhakikisha upanuzi wa barabara wa njia katika Mji wa Tunduma unatekelezwa kama ambavyo Ilani ya Uchaguzi Mkuu inavyoelekeza.
Amesema atamshauri Waziri wa Ujenzi kuhakikisha kunakuwa na mkandarasi ambaye atajenga kuanzia Tunduma ili wakutane kati na mkandarasi ambaye ameanza kujenga barabara ya njia nje mkoani Mbeya lengo likiwa ni kuwezesha ujenzi wa barabara kujengwa kwa kasi na hatimaye kuondoa changamoto ya msongamano wa malori.
“Wakati nakuja Tunduma nilikuwa namtafuta Waziri wa Ujenzi katika simu yake ili kuzungumza naye kuona umuhimu wa kuwa na mkandarasi ambaye atajenga kipande cha kuanzia hapa Tunduma.Hivyo nikirudi nitakwenda kuzungumza naye kuhusu hili.”amesema na kufafanua ujenzi wa upanuzi wa brabara hiyo tayari umeanza mkoani Mbeya.
Katika hatua nyingine Wasira ametumia nafasi hiyo kuzungumzia kuhusu malalamiko ya bodaboda kusumbuliwa na Polisi wa usalama barabarani ambapo amewataka bodaboda kupunguza makosa ya barabarani ili wasisumbuliwe lakini wakati huo huo Polisi nao kulegeza masharti kidogo ili wazungumze lugha moja.
Wananchi wakiwa katika mkutano huo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇