LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 18, 2020

ICHAGUENI CCM IKABORESHE SEKTA YA AFYA-DK MABULA

Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Ilemela, Dkt Angeline Mabula akielezea sera na mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano wakati wa mkutano wake wa kampeni katika uwanja wa stendi ya Pasiansi Kata ya Kawekamo hivi karibuni.
Sehemu ya umati wa wananchi ukiwa katika mkutan huo wa kampeni
Dk. Maula na mgomea udiwani wa Kata ya Kawekamo wakitamulishwa kwa wananchi


Na Mwandishi wetu, Ilemela.
 

Katika kipindi cha miaka mitano Serikali ya CCM imefanikiwa kuboresha sekta ya afya,hivyo wananchi wa Jimbo la Ilemela wamehimizwa kujiunga na bima za afya ili kupata huduma ya matibabu kwa urahisi na uhakika.

 

Kwani hakuna aliye na mkataba na Mungu kuwa ni lini ataugua na atakuwa katika hali gani ya kipato hivyo baada ya kuona changamato ya wananchi wengi kushindwa kugharamia matibabu pindi wanapopatwa na maradhi kutokana na hali ya uchumi Rais Magufuli aliboresha huduma ya bima ya NHIF kwa kuanzisha kifurushi cha mtu mmoja mmoja bila kujali ajira yake pia CHF ilioboreshwa inayotoa fursa ya familia ya watu 6 kupata matibabu kwa kuchangia kiasi cha 30,000.

 

Hayo yamesemwa na Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) jimbo la Ilemela,Dkt Angeline Mabula wakati wa mkutano wake wa kampeni katika uwanja wa stendi ya Pasiansi Kata ya Kawekamo amesema serikali imeboresha huduma ya afya na matibabu yanapatika,unapo zungumzia uwekezaji katika maeneo mbalimbali pia wanazungumzia na uwekezaji  katika  afya,hivyo wananchi wakate bima ili wakati wowote wanapojisikia vibaya ikiwemo kuumwa kichwa anenda kituo cha afya kwa ajili ya tiba bila ya kuwaza gharama za matibabu.

 

"Hakuna mwenye mawasiliano na Mungu ya kujua lini ataugua na atakua katika hali gani kiuchumi, kwa kulitambua hilo Serikali ya Dkt.Magufuli ilikuja na hoja ya msingi na nzito ya watu kupata huduma ya afya kulingana na kipato chao kupitia bima ya afya ya  NHIF na CHF ilioboreshwa ambayo inatoa fursa ya familia ya watu 6 kutibiwa  kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya Mkoa kwa gharama ya 30000 kwa mwaka mzima," amesema Dkt.Angeline.

 

 

Amesema kwa kuboresha sekta hiyo vifo vya mama na mtoto vimepungwa sana jimboni Ilemela na taifa kwa ujumla kwa sababu ya kuboresha huduma katika maeneo hayo pamoja na ongezeko la dawa ambazo zinapatikana kwa asilimia 98.

 

Hata hivyo aliwaahidi wananchi wa Kata ya Kawekamo kuwa endapo watamchagua Rais,Mbunge na Diwani anayetokana na CCM na wakashinda katika uchagu mkuu kwa utaratibu ule ule wa utatu  watajenga zahanati ya kata hiyo.

 

Sanjari na hayo kupitia mkutano huo aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji Wilaya ya Ilemela  na Katibu Mwenezi Wilaya ya Ilemela wa CHADEMA Johanes Emmanuel,alijiunga na chama cha CCM kwa madai kuwa haoni sababu ya kubaki alipo kuwa wakati mambo yanayofanywa na CCM yanaonekana na kufurahishwa na utendaji kazi wa awamua ya tano.

 

"Tulikuwa tunadai vituo vya afya tumeshuhudia Serikali ya awamu ya tano ikijenga,miundombinu ikiboreshwa,usafiri wa majini ikiwemo kivuko cha MV.Ilemela, shule zimejengwa na kuboreshwa mfano kisiwa cha Bezi kulikua hakuna shule  ila kupitia Dkt.Angeline sasa watoto wanasoma,nimeona aibu ndio maana nimerudi CCM," amesema Emmanuel.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages