Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani leo,Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto ,Mhe.Ummy Mwalimu amesema kiwango cha maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukoma umepungua kutoka watu 43 kati ya watu milioni Moja 2014 hadi watu kufikia wagonjwa 26 kati ya watu milioni Moja mwaka 2019.
Amezungumza hayo jana jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wazee ambao ni waathirika wa ugonjwa wa ukoma katika kijiji cha Samaria Kata ya Hombolo bwawani.
Amesema kupungua kwa maambukizi hayo ni kutokana na juhudi zaa serikali za kuhakikisha wanapima na kutoa matibabu bure kwa aathirika wa ugonjwa wa huo.
Pia Waziri Ummy amesema maambukizi mapya Ukoma kwa watoto takriban asilimia 41 % ambapo mwaka 2014 kulikuwa na watoto 90 na wamepungua hadi watoto 53 mwaka 2019.
Kwa upande wake mkurugenzi wa progamu wa elimu vijini (CHEP) Ruteni Kanal Msaafu Daudi Tandila amesema Kulingana na Takwimu hizo,na msimamo wa shirika la afya Duniani (WHO) yakuwa Kati ya wagonjwa elfu kumi akipatikana Mgonjwa Mmoja,italeta ripoti ya kuwa hakuna ugonjwa wa ukoma.
Hivyo Wizara ya afya ikusanye taarifa upya kupata Takwimu zinazotolewa na WHO za udhibitisho wa Kutokuwepo kwa ugonjwa huo.
Sambamba na hayo Waziri Ummy amekabidhi sukari kilo 50,Mchele kilo 100,maharage kilo 50,unga kilo 50 na viatu pea 48 kwa waathirika wa Ukoma kama ishara ya kuwathamini huku akishikana mikono nao katika kupinga dhana potofu ya kwamba ugonjwa huo unaambukiza kwa njia ya kushikana.
Kuhusu changamoto ya miundombinu ya barabara iliyopo katika eneo hilo Waziri Ummy amemwagiza mkuu wa wilaya alifanyie kazi kwani imekuwa kero na changamoto kubwa ambapo ilisababisha msafara wake kukwama mara kwa mara hali iliyomsababisha kutembea kwa miguu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇