Juhudi za uokozi bado zinaendelea katika mji wa Elazig kufuatia tetemeko la ardhi la kipimo cha Richter 6.8, lilopiga mashariki mwa Uturuki. Watu wapatao 29 wamepoteza maisha huku wengine kadhaa wakiwa bado wamekwama chini ya vifusi vya majumba yaliyoporomoka, hayo ni kulingana na taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Suleyman Soylu. Waziri huyo ameongeza kwamba zaidi ya watu 15,000 wamekimbilia kwenye vituo vya muda vya kuwahifadhi watu ikiwa ni pamoja na kumbi za michezo na za vyuo vikuu. Watu wengine 5,000 wamejihifadhi katika mahema. Wengine wapatao 1,500 wamepelekwa hospitalini kwa matibabu huko mjini Elazig pamoja na miji mingine jirani. Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa ni wilaya ya Sivrice ya Elazig, lakini pia lilitikisa maeneo ya miji mengine ya karibu.
Your Ad Spot
Jan 26, 2020
WATU 29 WAPOTEZA MAISHA TETEMEKO UTURUKI
Tags
featured#
Kimataifa#
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
Kimataifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇