Rais wa China Xi Jinping amesema idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya corona imefikia watu 56. China pia imetangaza vikwazo zaidi katika sekta ya usafiri. Zaidi ya watu 1,400 wameambukizwa virusi hivyo duniani kote, wengi wao nchini China. Hong Kong imetangaza hali ya dharura na kuzuia sherehe za mwaka mpya wa Kichina pamoja na safari za kwenda China bara. Australia imethibitisha visa vinne vya maambukizi, huku Canada ikithibitisha kisa chake cha kwanza hapo jana. Baada ya Malaysia kuthibitisha maambukizi ya watu wanne na Ufaransa Ijumaa kuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kukumbwa na maambukizi ya virusi hivyo. Marekani imepanga kutuma ndege maalumu hii leo kuwarejesha raia wake pamoja na wanadiplomasia kutoka mji wa Wuhan nchini China kulipoanzia virusi hivyo.
Your Ad Spot
Jan 26, 2020
IDADI YA VIFO VYA WATU 56 WAPOTEZA MAISHA CHINA VIRUSI CORONA
Tags
featured#
Kimataifa#
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
Kimataifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇