LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 14, 2019

CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI KIBONDO WANANCHI WATOA OMBI KWA SERIKALI DK.JOHN MAGUFULI

Na Said Mwishehe-Kibondo

Wananchi wa  Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, eneo la Station One wameiomba Serikali inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kuwasaidia kutatua changamoto ya uhaba wa maji.

Wakizingumza na Michuzi Blog leo Desemba 14 mwaka 2019, wananchi hao wamesema maji ndio kero kubwa kwao na kwamba wanaimani na Serikali Ikisikia kilio chao itatafuta Ufumbuzi ili waondokane na changamoto hiyo ambayo wamekuwa nayo kwa muda mrefu.

Akizungumza zaidi kuhusu changamoto ya kukosekana kwa maji ya kutosha Mkazi wa Station One Ali Kasato amesema wanalazimika kufuata maji umbali wa wa zaidi ya  kilometa mbili kutoka katikati ya maji yanayopatikana.

Amesema kuwa dumu moja la maji lenye ujazo wa lita 20 linauzwa Shilingi 700 kutokana na umbali wa kuyafuata  maji hayo kwa kutumia usafiri wa baiskeli.

"Kilio chetu kikubwa hapa kwetu Kibondo ni uhaba wa maji, ni Kweli kuna changamoto nyingine makini hizo angalau kidogo tunao uwezo wa kuzitatua wenyewe lakini kwenye shida ya maji hili limetuzidi uwezo, hivyo Ombi letu Kwa Serikali itusaidie Ili tuwe na maji ya uhakika.

"Maji tunayotumia sasa ni ya Chemchem ambayo ni salama kwani yalipimwa na wataalamu na kisha wananchi tukaelezwa yapo Salama. Hivyo hata kama watafanya utaratibu wa kutuvutia maji kutoka yalipo yakaja Mjini itatusaidia,"amesema.

Aidha ameshauri iwapo itawezekana Serikali ya Wilaya ya Kibondo kwa Kushirikiana na Serikali Kuu iwaruhusu wananchi kuchimba Visima vingine vya maji ili kupunguza msongamano wakati wa kuchota maji,"amesema.

Hata Hivyo amesema siku za karibuni walikuwa na kikao na viongozi wa Wilaya y Kibondo kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo ambapo walihakikishiwa na viongozi kuwa wataangalia uwezakano wa kutoa kibali chha kuchimbwa visima vingine viwili Ili kupunguza adha hiyo.
 
Sehemu ya madumu ya maji ambayo hutumika kubebea maji kutoka chemuchemu iliyopo umbali wa kilometa mbili kutoka eneo la Stesheni One wilayani Kibondo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages