LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 29, 2024

M-NEC ASAS AWATAKA VIJANA UVCCM KUMSEMEA RAIS DK. SAMIA, AKERWA NA UPOTOSHAJI VYAMA VYA SIASA

Ihemi, Iringa, Septemba 29, 2024.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Salim Asas amewataka vijana  wote nchini kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa  kazi kubwa anayoendelea kufanya ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Asas amesema hayo wakati akifunga mafunzo maalum kwa vijana 370 kutoka Kata 107 mkoani Iringa yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa, na kuhitmishwa leo Septemba 29, 2024 katika Chuo cha Ihemi.

Mafunzo hayo yaliyoanza septemba 23-29 yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo vijana katika kukilinda Chama na viongozi wake  yamehudhuriwa na vijana wapatao 370  kati ya 428 ya vijana wote ambao walitakiwa kushiriki, huku  kila kata ikitakiwa kutoa vijana wanne ambao ni Mwenyekiti na Katibu, Katibu wa Hamasa na mjumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM mkoa.

Akizungumza na vijana hao, Asas amesema wapo wanasiasa ambao wanaipotosha jamii kwa kueleza uongo juu ya utendaji kazi wa Rais Dk.Samia kwenye mitandao ya kijamii, na kuwataka  vijana hao kutowafumbia macho  watu wenye nia ovu na serikali wakiwemo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakisambaza maneno ya kichochezi yenye lengo la kuwachonganisha wananchi na serikali yao.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia imefanya kazi kubwa kuanzia miradi ya kimkakati  na  ya maendeleo kuanzia ngazi ya Kata, Vijiji na Vitongoji kwa kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi pamoja na kutekeleza miradi mipya, hivyo ni jukumu la  vijana wa UVCCM kuhakikisha wanaitumia  vizuri mitandao ya kijamii kujibu upotoshaji huo kwa kusemea  juu ya kazi kubwa ya utekelezaji wa Ilani  inayofanyika.


‘’Wapinzani baada ya kuona kila wanapogusa mama kafanya, kila wanapotaka kupotosha mama katekeleza wamefilisika ajenda na hivi sasa wameamua kumchafua kiongozi wetu mkuu kwa kueneza uongo, haiwezekani tunyamaze. Na sisi tunataka asilimia 70 ya majibu ya kumtetea kiongozi wetu,hivyo  vijana tunahaja ya kumsemea mama,tumieni mitandao ya kijamii kujibu upotosha unaofanywa na vyama vya upnzani’’amesisitiza Asas.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Salim Asas akizungumza wakati akifunga mafunzo maalum kwa vijana 370 kutoka Kata 107 mkoani Iringa yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa, na kuhitmishwa leo Septemba 29, 2024 katika Chuo cha Ihemi.
Wahitimu wakimsikiliza MNEC Asas.

MNEC Asas akigawa vyeti wa wahitimu👇





Wahitimu wakiwa ukumbuni👇



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages