Sehemu ya umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja Geita Mjini Agosti 13, 2024.
Dk Nchimbi na msafara wake wakiingia kwenye mkutano huo.
Dk Nchimbi akihutubia katika mkutano huo ambapo amesisitiza watanzania kudumisha mila na destuli ikiwemo kulinda maadili lakini pia amewaasa viongozi wa vyama vya siasa kuchunga ndimi zao kwa kutotoa lugha za kichochezi zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani ya nchi.
Dk Nchimbi amehitimisha ziara yake ya siku 3 mkoani Geita ambayo ilianza Agosti 11 baada ya kutokea ziara ya Mkoa wa Kagera.
Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
Balozi Dk. Nchimbi, katika hiyo ziara ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) - Oganaizesheni, Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid.Dk Nchimbi akijadiliana jambo na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla.
Msanii Magambo akitumbuiza wakati wa mkutano huo.
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema na kuhamia CCM, Upendo Peneza akieleza sababu zilizomfanya ahamie ikiwemo uongozi bora wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Dk. Nchimbi akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella kablasha la kero za wananchi ili azitatue.Kero hizo zimetolewa na wananchi wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo akijibu baadhi ya kero za mkoa huo ikiwemo upungufu wa magari ya zimamoto na magari ya viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani huo. Amewaondolea hofu kwa kuwaeleza kuwa serikali imeagiza magari hayo na mkoa huo kupata mgawo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya akijibu baadhi ya maswali na kueleza kuhusu ujenzi wa barabara unaoendelea mkoani humo.
Dk Nchimbi akipokea kadi 66 za waliokuwa vyama vya upinzani na sasa wamehamia CCM.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇