Imewekwa na Dismas Lyassa
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi kitaendelea na msingi yake ya kudumu ya kujenga Amani, Umoja na Mshikamano na kuwahimiza wana CCM kuwa wastahamili wakati huu kuelekea Uchaguzi Ujao.
Dk.Mwinyi ameyasema hayo juzi tarehe 12 Agosti 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na Wajumbe wa Kamati za Siasa za Wadi, Tawi, Jimbo, Wilaya na Mkoa za Mkoa wa Kusini kichama katika ukumbi wa Dkt.Ali Mohamed Shein, Tunguu.
Aidha Dk.Mwinyi amewanasihi Viongozi wa Vyama vya Siasa kuacha kuhubiri Siasa za chuki na badala yake kuhubiri Amani kwa dhamira ya kuimarisha Amani ya nchi.
Halikadhalika Dk.Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kwa asilimia mia moja katika utekelezaji wa Ilani na kuwahimiza wananchi kuunga mkono hatua hiyo.
Pia ameeleza kuwa Serikali bado ina mpango wa kujenga barabara ya kisasa kuanzia Tunguu hadi Makunduchi yenye urefu wa takriban kilomita 43. Barabara hiyo itakuwa ya njia nne na yote itafungwa taa.
Kwa upande mwingine Dk.Mwinyi amewasisitiza wana CCM kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga kura ili kuwa na sifa ya kushiriki Uchaguzi mkuu mwakani na kukihakikishia Chama cha Mapinduzi Ushindi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇