Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, anaendelea na Kampeni ya Sensa ya Watu na Makazi Jimboni mwao.
Kila afanyapo Kampeni hiyo, anatathmini Maendeleo yaliyopatikana ndani ya miaka kumi (10), yaani, 2012-2022, na umuhimu wa Sensa (takwimu za watu na makazi) kwenye Kata (vijiji & vitongoji vyake) husika.
KATA ILIYOKUWA HAINA SEKONDARI YAISHUKURU SERIKALI YETU
Kata ya Ifulifu ilikuwa Kata pekee ndani ya Jimbo letu isiyokuwa na Sekondari yake. Kwa sasa Kata hiyo inazo mbili zitakazofunguliwa Januari 2023.
IFULIFU SEKONDARI
Sekondari hii imejengwa Kijijini Kabegi kwa mchango mkubwa wa Serikali yetu iliyochangia Tsh Milioni 470 (Tsh 470m) na bado itaendelea kuchangia.
Shukrani nyingi sana zimetolewa kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan - sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.
Wanavijiji na Viongozi wao, akiwemo Mbunge wa Jimbo, nao wamechangia ujenzi wa Sekondari hii ya kisasa na yenye maabara 4 (physics, chemistry, biology & geography).
Sekondari hii itafunguliwa Januari 2023
NYASAUNGU SEKONDARI
Sekondari hii inajengwa Kijijini Nyasaungu kwa nguvukazi na michango ya fedha taslimu za Wanakijiji wa Nyasaungu, Viongozi wao akiwemo Mbunge na Jimbo. Mfuko wa Jimbo nao unachangia ujenzi huu.
Sekondari hii itafunguliwa Januari 2023
UJENZI WA "HIGH SCHOOLS" ZA MASOMO YA SAYANSI NDANI YA JIMBO LETU
Wakati tunamalizia kiu ya kuwepo kwa Sekondari 1 hadi 2 kwa kila Kata (tunazo Kata 21) kifuatacho ni ujenzi wa "High Schools" za masomo ya Sayansi Jimboni wetu - kazi hii imeanza!
Usiache kusikiliza CLIP/VIDEO iliyoko hapa, na usiache kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumamosi, 20.8.2022
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇