LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 20, 2022

KWA NIABA YA RAIS, RIDHIWANI AKABIDHI MASHAMBA 11 KWA WANANCHI KILOSA

 

   

Picha mbalimbali Ridhiwani Kikwete akiwa wilayani Kilosa


Na Mwandishi wetu…
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Ridhiwani Kikwete amewahimiza viongozi wa Wilaya ya Kilosa kusimamia mpango wa matumizi ya mashamba 11 aliyoyakabidhi Mwishoni mwa wiki , Wilayani humo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan. 

Naibu Waziri Kikwete aliwashukuru wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kushirikiana na Rais Samia katika maendeleo.

“Na hii ndiyo sababu Rais ameona kipaumbele kikubwa ya mashamba hayo kiwe ni wananchi ambao amewaomba mjiunge kwenye vikundi vya Ushirika ili mtumie kwa ajili ya Kilimo chenye tija”Alifafanua Waziri Kikwete.

Kwa upande wa Wakazi hao, walimshukuru na kumpongeza Rais kwa kuwapatia mashamba hayo na wakaahidi kuyatumia kama walivyoelekezwa.

Hata hivyo Ridhiwani ameeleza ziara yake inayohusiana na utatuzi wa migogoro ya ardhi itaendelea baada ya Zoezi la Sensa tarehe 23 Agosti 2022. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages