Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dorothy Kilave akishiriki kuchanganya zege, baada ya kukuta ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa ukipamba moto katika Shule ya Diplomasia, alipofanya ziara ya kukagua miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Kata ya Kurasini jimboni humo, jana. Anayesaidia kumwagilia maji ni Naibu Meya wa Temeke ambaye ni Diwani wa Kata hiyo ya Kurasini Arnold Peter. Ujenzi wa vyumba hivyo unagharimu sh. milioni 240. Sanjari na ujenzi wa madarasa hayo yanajengwa matundu 10 ya vyoo kwa gharama ya sh. milioni 15. Mbunge Kilave amesema fedha zote za ujenzi huo zimetolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Mtiririko wa ziara👇
Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dorothy Kilave akizungumza na Viongozi wa Mashina na Watendaji wa Chama na Serikali alipofanya nao kikao katika Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Chang'ome, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Kata ya Kurasini jimboni humo, jana. Kushoto ni Diwani wa Kata hiyo Kelvin Mhozye.Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Baada ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo Maendeleo na changamoto mbalimbali katika Kata ya Chang'ombe, Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, akahititimisha kikao hicho.
Mbunge Kilave na msafara wake wakafika Shule ya Msingi Unubini
Mbunge Kilave akilakiwa na uongozi kwa furaha baada ya kuwasili katika Shule ya Unumbini
Mbunge Kilave akaingia Ofisini kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Unubini Kata ya Chang'ombe na kabla ya yote akatia saini kitabu cha Wageni. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Cecilia Kweka.
Afisa Mtendaji Kata ya Chang'ombe Anzamen Nandari akimkaribisha Mwalimu Mkuu kuzungumza na kuwatambulisha walimu kwa Mbunge Kilave.
Mbunge Kilave akiwatazama Walimu wakati wakijitambulisha kwake, mmoja baada ya mwingine. Shule hiyo ina jumla ya Walimu 22.
Kisha Mbunge Kilave akasomewa risala ambapo katika risala hiyo yalitanjwa mafanikio ya shule ikiwemo kufaulisha wanafunzi kwa asilimia 100 katika mitihani iliyopita ya kuhitimu darasa la saba na kisha kutajwa kero ikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo, vitendea kazi ikiwemo samani na mazingira yasiyokuwa wezeshi vya kutosha kwa Walimu.
Mbunge Kilave akipitia kwa makini kero zilizotajwa baada ya kukabidhiwa risala.
Kisha Mbunge Kilave akazungumza na walimu hao. "Kwanza hongereni kwa mafanikio ya kufaulisha vizuri watoto kwa asilimia 100, lakini pia changamoto mlizowasilisha nimezipokea, kwa kweli zimenigusa sana, baadhi nitazifanyia kazi na nyingine nitazifikisha kunakohusika ili ionwe namna zitakavyoweza kupatiwa ufumbuzi, poleni sana.", akasema Mbunge Kilave.
Kisha Mbunge Kilave akawakabidhi rasmi Mwalimu Mkuu na Mtendaji, viti vitano vya kisasa vilivyonunuliwa kwa fedha alizotoa kuisaidia shule hivi karibuni.
Halafu ukafuatia ukaguzi wa Vyoo👇
"Kwa hiyo sasa pale kwenye choo kile maji yapo au hamna?", akauliza Mbunge Kilave akajibiwa hayapo ila wanafunzi hutakiwa kuingia nayo, hapa shuleni yapo.Mbunge Kilave akatoka kukagua vyoo vya Wanafunzi wa kike
Kisha akashuhudia vyoo vya Wanafunzi wa Kiume
"Kwa kweli hili suala la vyoo itabidi lifanyiwe kazi", Mbunge Kilave akasema wakati akitoka kukagua vyoo vya Wanafunzi na Walimu wa shule hiyo ya Unubini.
Kisha akamkuta Mama mjasiriamali akiuza bidhaa ndogo ndogo shuleni hapo👇
"Sasa watendaji wa Mitaa na Kata wa CCM na serikali, inapaswa mfanye jitihada za makusudi kuhakikisha wajasiriamali kama hawa wanapata mikopo, na jitihada zenyewe ni kuwafikia na kuwaeleza inakopatikana na namna ya kuipata, msisahau kuwa hawa ndiyo wanaotufanya tuwe viongozi na tunakuwa viongozi ili kuwasaidia", akasema Mbunge Kilave. Kisha akaendelea kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule hiyo👇
"Ujenzi naona unaenda vema, basi watendaji endeleeni kusimamia vizuri ili ujenzi huu ukamilike kwa kiwango kinachostahili", akasema Mbunge Kilave.
Mbunge Kilave akiingia katika Ofisi ya Walimu kukagua hali ya mazingira yalivyo.
"Enheee, jamani kwa hiyo sakafu ndivyo hivi ilivyo, ohh, hapana hii lazima iboreshwe ilingane na hadhi ya Ofisi ya Walimu", akasema Kilave huku akiahidi kusaidia kupatikana ufumbuzi wa kuboreshwa ofisi hiyo ya walimu.
"Hii ndiyo Kabati ya Walimu", Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Unubini akamwambia Mbunge Kilave.
"Na Kutokana na uhaba wa samani, ikiwemo viti baadhi ya walimu inabidi watumie madawati, kama hili", akasema Mwalimu Mkuu huyo.
Mbunge Kilave akitoka katika ofisi ya Walimu huku akionekana kutafakari sana mazigira aliyoona. Kisha akasalimia na kuzungumza na wanafunzi waliokuwepo.👇
"Watoto wangu, Mimi Mbunge wenu Kilave, nawaomba msome kwa bidiii, waheshimuni walimu. Tazama mnato nyumbani wazazi bado wamelala na mlirudi nyumbani jioni mnakuta wazazi hawajarudi kutoka kazini, mnakutana nao wakati wa chakula na mkizungumza kidogo inafika wakati wa kulala, kwa hiyo Wazazi mnaokuwa nao mda mrefu sana ni Walimu, wapendeni na waheshimuni sana", akasema Mbunge Kilave.
"Nani anataka kuwa kama Rais Samia", Mbunge Kilave akawauliza wanafunzi hao. nao wakainua mikono kuashirikia kuwa kila mmoja anapenda kuwa kama Rais Samia bila kujadi ni mwanafunzi wa kiume au wa kike!
Kumbe wanafunzi hao walikuwa wameshadokezwa kuwa Mbunge Kilave amefika shuleni kwao ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa! Wakamwimbia wimbo wa 'Happy Birthday'
Kisha Mbunge Dorothy na Diwani wa Kata ya Chang'ombe na wa Viti Maalum wakapata picha ya kumbukumbu.
Watoto wakafurahi mnooo!
Baada ya kuona walivyofurahi, Mbunge Kilave akamkabidhi Mwalimu Mkuu fedha kiasi, ili awanunulie juisi kwa ajili ya Birth Day yake.
KATA YA KURASINI👇
Mbunge Kilave akisaini Kitabu cha wageni kabla ya kuanza kuzungumza na wajumbe.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kurasini Chacha Togocho akifungua kikao hicho.
Wajumbe wakisubiri kumsikiliza Mbunge Kilave
Mbunge Kilave akiwasalimia wajumbe na kuzungumza nao katika kikao hicho.
"Jamani baada ya kuwasalimia naomba nziungumze nanyi nikiwa nimekaa", akasema Mbunge Kilave.
Mbunge Kilave akaaza kuzungumzia masuala mbalimbali na wajumbe.
"Mnajua kuna mambo mnaweza kujikuta ninyi wajumbe wa mitaa hamyajui yanayoendelea kumbe tatuzo ni ninyi wenyewe. Mimi Mbunge nikishapata mambo nayafikisha kwa Diwani naye anayafikisha kwa viongozi wa Mitaa kwa njia ya vikao, sasa kama usipohudhuria vikao hivyo, utayajuaje?," alisema na kuwahoji Mbunge Kilave.
"Lazima viongozi na wananchi muwe wafuatiliaji, msidhani kuna mtu atapita kuwajulisha kila kitu nyumba hadi nyumba, hudhurieni vikao vinapoitishwa, maana kuna mambo ya maendeleo kama ya mikopo, haya msipoyafuatilia mtakuwa kila mara mnadhani mmebaguliwa, kumbe siyo", akasema Mbunge Kilave, huku akiwataka viongozi wa Mitaa nao kuwa makini katika masuala ya mikopo kwa kuhakiki majina ya waombaji kupitia vikundi, kwa kuwa baadhi ya waombaji huweza kujipatia fedha nyingi za mikopo kwa njia za udanganyifu wa kuweka majina bandia katika orodha ya kikundi hadi kufikia watu 20 kumbe ni watu watatu tu.
Diwani wa Kata ya Kurasnini akijibu baadhi ya Kurasini na Naibu Meya wa Temeke Arnold Peter akifafanua baadhi ya mambo yaliyokuwa yanajiri kwenye kikao hicho.
Kiongozi wa Mtaa akieleza changamoto katika kikao hicho.
Afisa Maendeleo Kata ya Kurasini Tina Muzo, akifafanua jinsi mikopo ya Halmashauri inavyopatikana baada ya mmoja wa wajumbe kueleza kuwa ni migumu kupatikana kutokana na masharti kuwa mengi. "Mheshimiwa Mbunge, tatizo hapa ni kwamba waombaji mikopo wengi katika kata hiyi wanataka mikopo ya muda mfupi siyo ya muda mrefu, sasa inakuwa vigumu mtu kupatiwa sh milioni 20 kwa kumwangalia sura tu, lazima atoe vielelezo na udhamini wa kutosha ndiyo apatiwe mkopo", akafafanua Afisa maendeleo huyo.
Kisha msafara ukaondoka kwenda kukagua miradi ya ujenzi wa Madarasa shule ya Diplomasia
Kisha Mbunge Kilave akakabidhiwa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo.Mbunge Kilave akitoka kukagua ujenzi wa chumba cha darasa kati ya vyumba 12 vinavyojengwa katika shule hiyo ya Diplomasia
"Kwa hiyo hii mashine ya 'Photocopy' inafanya kazi vizuri?" akauliza Mbunge Kilave wakati anakagua mashine hiyo ambayo imegharimu sh. milioni 2.2 kutoka fedha za mfuko wa jimbo. Wapili kulia ni Mkuu wa shule hiyo ya Diplomasia.
Kisha Mbunge Kilave akaenda Shule ya sekondari ya Uhamiaji kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo👇
Mbunge Kilave akikagua saruji inayotumika katika ujenzi huo
Akakagua na mbao zinazotumika katika ujenzi huo.
Kisha akasaini kitabu cha wageni mbele ya Mwenyeji wake, Mkuu wa shule hiyo ya Uhamiaji Rehema Akwilombe.
Mbunge Kilave akizungumza kuhusu maendeleo ya ujuenzi wa madarasa hayo na Mkuu wa Shule ya Uhamiaji Rehema Akwilombe (kulia).
Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akihitimisha ziara yake kwa kuzungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo ya Sekondari ya Uhamiaji, ambapo aliwafunda mambo mbalimbali ikiwemo kusoma kwa bidii na kujichunga sana wasipate mimba wangali masomoni. "Wanangu, japo imekubalika kuwa unaweza kurejea masomoni baada ya kujifungua ukipata nani hii.., lakini jitahidini sana, sana, sana, ikitokea iwe ni bahadi mbaya sana, msifanye makusudi mtaharibu maisha", Mbunge Kilave, akawafunda wanafunzi hao.
©2021 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇