LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 7, 2021

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR AFUNGUA KITUO CHA UMAHIRI CHA MAGONJWA YA MOYO NA MISHIPA YA DAMU MLOGANZILA.

  Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki (The East African Centre of Excellence for Cardiovascular Sciences) cha Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili katika kampasi ya Mloganzila. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

Na Mwandishi wetu.

Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman amefungua Kituo cha Afrika Mashariki cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu (The East African Centre of Excellence for Cardiovascular Sciences) cha Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila.

Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa Kituo hicho kilichojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Mhe. Othman alisema amefurahishwa na maendeleo yaliyopatikana tangu mazungumzo ya awali ya uanzishwaji wa Kituo hiki yalipofanyika mwaka 2012 kwa kuwa na mwazo mazuri na leo sote nimashahidi. 

Alisema kuwa anaamini uwekezaji uliofanyika ni wa faida kubwa kwa Serikali na kwa wananchi pia hasa ukizingatia takribani kila kaya hapa nchini imeathirika na magonjwa haya ya moyo na Kituo hiki kimekusudia kushughulikia matatizo hayo.

“Kituo hiki kitatoa mafunzo mbalimbali ya rasilimali watu wa afya ambayo wanahitajika kwa ajili ya kuzuia na kuhudumia magonjwa ya moyo na mishipa damu na kwa kufanya hivyo, tutaweza kukabiliana na changamoto ya upungufu wa rasilimali watu wanaohitajika katika maeneo haya”, Mhe Othman aliongeza.

Ufunguzi wa Kituo cha Afrika Mashariki cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwa ni pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali na mwakilishi kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika.

Kwa mujibu wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof. Joyce Ndalichako Kituo hiki kimejengwa kimkakati katika kampasi hii ya Mloganzila na kinalenga kukuza ujuzi na elimu ya juu katika sayansi za biomedikali (Skills Development and Tertiary Education in Biomedical Sciences) ili kuweza kuchangia katika maendeleo ya watumishi wanaohitajika na wenye ujuzi wa hali ya juu katika sayansi za biomedikali na hivyo kukidhi mahitaji ya haraka ya soko la ajira la Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

“Katika kufanikisha mradi huu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliingia mkataba wa mkopo kwa masharti nafuu na Benki ya Maendeleo ya Afrika ambapo Benki ilitoa TZS 18,623,125,000.00 ikiwa ni sawa na asilimia 92.58 na Serikali ya Tanzania iliridhia kutoa TZS 1,489,850,000.00 ikiwa ni sawa na asilimia 7.42 kama ufadhili wa serikali” Prof. Ndalichako alieleza.

Sambamba na hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikihi, Muhimbili, Prof. Pembe alieleza kuwa kituo hiki kina vyumba vya madarasa, semina, ukumbi wa mikutano, kumbi za makongamano kwa njia ya video, chumba cha mafunzo kwa njia ya mtandao, maktaba, chumba cha takwimu, (data management centre), maabara nne kwa ajili ya tafiti, na za mafunzo kwa vitendo pamoja na  ofisi za wanafunzi wauzamivu na za wafanyakazi. 

“Katika kuandaa walimu watakaofundisha katika kituo hiki, mradi umetoa mafunzo kwa wataalam wapatao 38 na kati ya hao wataalam wapatao 29 wamemaliza na wanaendelea kutoa mafunzo na huduma katika taasisi mbalimbali za afya hapa nchini” Prof. Pembe alieleza.

Aliongeza kuwa pamoja na kwamba kituo hii kitakuwa chini ya Chuo, kitafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ili kutekeleza sera, taratibu na miongozo ya huduma za afya na wakati huo huo kikitekeleza sera, taratibu na miongozo ya Elimu ya juu kama zilivyoainishwa na Wizara zote mbili.

Aidha katika Ufunguzi wa Kituo hiki, Mhe Othman aliwasihi watanzania kujitahidi kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kugundua magonjwa mapema ili yaweze kutibiwa mara moja. Pia alisisitiza kuzingatia njia mbalimbali za kinga hasa kwa magonjwa ya moyo na mishipa damu ambayo ni ghali sana kutibu na yana kawaida ya kuwa na matokeo mabaya ikiwa hayatatibiwa kwa wakati.

 “Napenda kuchukua fursa hii kuwahakikishia wanajumuia wa MUHAS kwamba serikali itaendelea kuwaunga mkono katika kuhakikisha hospitali ya moyo ya kufundishia wataalam kwa vitendo inajengwa ili Kituo hiki kiweze kukamilika kama ilivyokuwa imepangwa,”, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliongeza.




Picha muonekano wa jengo
Baadhi ya wanafunzi waliofadhiliwa

  Baadhi ya viongozi waalikwa wakimsikiliza Makamu wa Rais Zanzibar (hayupo pichani) wakati wa  ufunguzi Kituo cha Afrika Mashariki cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu (The East African Centre of Excellence for Cardiovascular Sciences) cha Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili katika kampasi ya Mloganzila.
  Mhadhiri na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo na Watoto Idara ya Magonjwa na Afya za Watoto. Dr. Deogratias Nkya (kulia) akifafanua jambo mara baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (kulia)  alipofika katika moja ya chumba cha upasuaji wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki (The East African Centre of Excellence for Cardiovascular Sciences) cha Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila.
Mwenyekiti Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi Prof. Gideon Kwesigabo (kulia) akimuonesha ramani ya jengo Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (wa pili kushoto) wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki (The East African Centre of Excellence for Cardiovascular Sciences) cha Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila.

Mtaalam Mbobezi katika kuzibua mishipa ya Damu na Moyo (Cardiac Catheterization) Dkt. Lukas Mwaijega (wa pili kushoto) akizungumza na  Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (kulia) mara alipotembelea chumba kitakachotumika  kutoa elimu ya hamasa ya kinga na ukarabati kwa vitendo kwa waathirika katika mashine zitakazo fungwa kuhudumia wateja 40 kwa wakati mmoja. 

Baadhi ya viongozi wakiimba wimbo wa Taifa akiwepo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mwanaidi Ali Khamis (wa kwanza kushoto)  
Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (wa pili kulia) akishirikiana na baadhi ya viongozi kukata utepe kuashiria ufunguzi huo 
Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (wa pili kulia) akifunua jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa jengo hilo
  
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiimba wimbo wa Taifa


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili. Prof. Andrea Pembe akizungumza katika hafla hiyo
Mkurugenzi Bendi ya Mjomba na msanii wa muziki wa dansi, sanaa ya jukwaani Mrisho Mpoto akisherehesha katika hafla hiyo



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akizungumza akizungumza jambo wakati wa ufunguzi Kituo cha Afrika Mashariki cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu (The East African Centre of Excellence for Cardiovascular Sciences) cha Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila.
 
Mwenyekiti Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Harson Mwakyembe akitoa salamu za chuo hicho kwa Mgeni rasmi 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza jambo  


Wanahabari wakiwa kazini
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Prof. Appolinary Kamuhabwa akito  neno la shukrani





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages