SPIKA wa Bunge, Job Ndugai akihutubia wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Azaki leo katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma. |
Baadhi ya wadau wa Asasi za kiraia kiraia wakisikiliza kwa makini wakati Spika Ndugai akihutubia.
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amezitaka Asasi za kiraia (Azaki) kutumia tafiti na takwimu vizuri zitakazosaidia kutoa majawabu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya watanzania.
Wito huo umetolewa na Spika Ndugai wakati wa ufunguzi wa Wiki ya AZAKI (2021) jijini Dodoma leo ambapo amesema asasi hizo hazina budi kutafuta fedha ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuleta tija na vipaumbele vya taifa .
Aidha, Ndugai amezitaka Asasi hizo kufanya kazi kwa weledi,uadilifu na uzalendo kwa maslahi mapana ya taifa.
Ndugai amezitaka asasi hizo kuwa na mwenendo wa kukosoa viongozi wa serikali lakini pia wana wajibu wa kuwapongeza hasa pale wanapofanya vizuri wanapotekeleza majukumu yao kwa ajili ya maslahi ya watanzania wote.
Kwa upande wake rais wa Taasisi ya uwezeshaji asasi za kiraia (Foundation For Civil Societt- FCS) Dkt. Stigmata Tenga amesema ipo haja kwa bunge kuleta mabadiliko na kupitia upya sheria, taratibu na miongozo ambayo inaziongoza asasi hizo ili ziweze kushiriki vyema katika kutekeleza kazi zao na majukumu yao kwa maendeleo ya taifa.
Maonesho ya Wiki ya Azaki -2021) yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo Azaki na Maendeleo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇