LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 14, 2021

DIWANI MSTAAFU KULTHUM SAGAMIKO ATOA MSAADA WA MIFAA VYA USAFI SHULE SEKONDARI OYSTERBAY, AMFAGILIA RAIS SAMIA

CCM Blog, Oysterbay

Diwani mstaafu wa Msasani, viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kulthum Sagamiko amekabidhi msaada wa fagio 100 na mapipa kadhaa ya kuhifadhia taka katika Shule ya Sekondari ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, katika kutekelea Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020- 2021.

Akikabidhi msaada huo Kulthum ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji ya UWT Wilaya ya Kinondoni, amesema Wananachi hasa kina Mama wanatakiwa kuwa na utayari wa kuzisadia kuziboresha shule kimazingira ikiwa pia ni njia mojawapo ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Rais Mama Samia Suruhu Hassan katika kusukuma gurudum la maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Dickson Kajuna amemshukuru Diwani huyo na kusema amekuwa mfano bora kwa kuwa shule ilikuwa na uhitaji wa vifaa hivyo na kuahidi kuvitumia kulingana na makusudi na diwani huyo.

Ziafuatazo ni picha mbalimbali, wakati Diwani Mstaafu Kulthum alipokuwa akaikabidhi msaada huo jana.










No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages