LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 14, 2021

MAADHIMISHO SIKU YA AFYA YA AKILI, KUTOKUNYWA POMBE DUNIANI YAFANA DODOMA



Mkurugenzi Msaidizi  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. James Kihologweakihutubia wakati wa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili na ya Kutokunywa Pombe Duniani iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya Mirembe jijini Dodoma Oktoba 10,2021.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fikrafya, Shabbirhussein Khalfan (wa pili kulia) akimkabidhi mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. James Kihologwe mfano wa mti wenye matawi yenye  maneno ya kumletea mtu furaha na faraja katika maisha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili na ya Kutokunywa Pombe Duniani iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya Mirembe jijini Dodoma Oktoba 10,2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Paul  Lawala akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoamua kuacha kunywa pombe wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili na ya Kutokunywa Pombe Duniani iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya Mirembe jijini Dodoma Oktoba 10,2021.
Mbunge wa Viti maalumu, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi, Salome Makamba akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ambapo ameiomba serikali ikipitishwa sheria ya Bima ya Afza kwa Wote wawakumbuke wagonjwa wa akili kupata bima.
Mwenyekiti wa MEHATA, Isack Lema akizungumza katika maadhimisho hayo kwa kuelezea mikakati mbalimbali ya taasisi hiyo.
Monica Isaya  aliyewahi ugua ugonjwa wa akili na kuponywa katika 
katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, akisoma shairi maalumu alililolitunga kwa muda mfupi kushukuru kwa huduma aliyopatiwa  
Rustika Tembele akitoa maelezo kuhusu kazi za taasisi yake wakati wa maadhimisho hayo.
Dkt. Kihologwe akipata maelezo namna Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (TGGA)  inavyoshirikiana na taasisi zingine kutoa elimu kwa wananchi ili waepukane na unywaji wa pombe wakati wa maadhimisho hazo. Kushoto ni Afisa Mipango wa TGGA, Valentina Gonza. Katikati anayetoa maelezo ni Mratibu wa chama cha Afya ya Jamii (TPHA).
Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Mwandabila akipima kimo chake katika banda la Hospitari ya Mirembe wakati wa maadhimisho hayo.
Dkt James akiwa banda la Hospitari ya Mirembe akipata maelezo kuhusu tiba zinazotolewa hospitalini hapo.

Baadhi ya wananchi wakiwa banda la TGGA na TPHA kupata maelezo jinsi ya kuepukana na unywaji pombe kupita kiasi.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Taanet, Gladnes Munuo akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.
Seehemu ya wananchi wakiwa katika maadhimisho hayo.




PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA




IMEBAINISHWA kuwa mpaka kufikia mwaka 2030 tatizo la afya ya akili  duniani litaongezeka  hadi  kufikia asilimia 17 kutoka asilimia 12 na endapo  jamii ikasimamia suala la malezi na makuzi tatizo hilo litapungua hadi kufikia asilimia 1.

Akizungumza katika kilele  cha maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani na kupinga matumizi ya pombe kupita kiasi October 10 Mkurugenzi Msaidizi  kutoka Wizara ya Afya anayeshughulikia Magonjwa yasiyoambukiza Dk James Kihologwe amesema suala la afya  ni mtambuka katika malezi na kila mmoja anao wajibu wa kufanya tatizo hilo lipungue

Aidha Kihologwe ameeleza kuwa suala la tatizo la afya ya akili huchangiwa na sababu nyingi ikiwemo na unywaji wa pombe uliopitiliza utumiaji wa madawa ya kulevya ,mawazo Sonona na sababu nyingine nyingi.

"Athari  ya pombe na madhara yake ni makubwa ambapo takwimu zinaonesha tuna tatizo kubwa la vifo Milioni 3 vinavyotokana na pombe duniani huku wengine wakiwa na ulemavu wa maisha," Amesema  Dk. Kihologwe. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo kuwa ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk.Shedrack Makubi amesema Takwimu zinaonesha Tanzania  kuna wagonjwa wa afya ya akili Milion 7.

"Tunatakiwa kuchukua hatua za haraka na kuwekeza zaidi katika Magonjwa ya akili, afya ya akili kwani tatizo hili limeonekana kukua siku hadi siku," amesema Dk. Makubi. 


Paul Lawala ni Mkurugenzi Mtendaji Hospital ya Taifa ya Afya ya akili Mirembe alibainisha kuwa licha ya jitihada zinazofanyika Bado Kuna changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa wataaluamu wa afya za akili.

Pia Alibainisha changamoto ya miundo mbinu ambayo iliyopo kwa Sasa haikidhi mahitaji ya huduma zinazotolewa kwani imechakaa hasa barabara zinazoingia sehemu za kutolea huduma.

Alitoa wito kwa jamii kuacha kuwanyanyapaa wagonjwa wa afya ya akili kwani ni wagonjwa kama wagonjwa wengine na wanastahili haki anazostahili mgonjwa yoyote na muwasihi  kuwapeleka kwenye vituo vya kutolea huduma mara waonapo dalili za ugonjwa.

"tunaomba Serikali itusaidie kuwasomesha wataalamu wa afya za akili Katika fani hiyo na kuwaajili huku wakipewa mazingira mazuri ya kazi jambo ambalo litasaidia  kurahisisha kazi"alisema 

Nae Mbunge wa Shinyanga viti maalumu,Salome Makamba  ameitaka jamii kuamimi kwamba ugonjwa wa akili unatibika na kuacha imani potofu za kuwapeleka wagonjwa kutibiwa kwa waganga wa kienyeji na badala yake wagonjwa wote wenye changamoto  hiyo wapelekwe katika hospitali ya Mirembe iliyopo Dodoma. 

"Kwenye jamii yetu bado tunachangamoto kubwa,ukweli usiopingika elimu juu ya magonjwa ya afya ya akili ni mdogo na wengi hudhani kwamba ukipata tatizo la akili huwezi kupona jambo ambalo sio la kweli,

"Sasa hivi Serikali  ipo kwenye mchakato kupitisha muswada ili iwe sheria ya bima ya afya kwa  kila mtanzania lazima awe na bima ya afya na mimi kama mbunge mwakilishi wa wananchi napendekeza ugonjwa wa akili uingie kwenye matibabu ya bima ya afya,"amesema Salome



 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages