Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge akiongoza kupanda miti eneo la Hospitali mpya
ya Uhuru wilayani Chamwino mkoani
humo siku ya maadhimisho ya Mapinduzi Tukufu
ya Zanzibar Januari 12, 2021.
Mkuu wa
Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyakoga
akishiriki kupanda miti eneo la Hospitali ya Uhuru.
Diwani wa Kata ya Buigiri ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Kenneth Yindi akipanda mti katika eneo la Hospitali ya Uhuru ambayo ipo katika kata hiyo.
Dkt. Mahenge akjadiliana jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy wakati wa kazi hiyo ya kupanda miti ikiendelea.
Mwanafunzi wa Udom, Mariam Hamza akipanda mti.
Mwanafunzi Raphaela William wa UDOM, akiungana na wanafunzi wenzie wa Kitivo cha Elimu COED kupanda miti katika eneo hilo.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa CCM, Chuo Kikuu cha Dodoma Kitivo cha Elimu, Godfrey
Masele (kushoto) na Katibu Mkuu wa UVCCM wa Kitivo hicho, Faris Burhan wakisaidiana kupanda mti katika eneo hilo la Hospitali pamoja na
wanafunzi wenzao 198.
Mwanafunzi Debora Adrian (kushoto) akisaidiana na mwenzie kupanda mti.
Mwanafunzi Maida Abubakar akiwa makini kupanda mti.
MKUU wa Mkoa
wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge ametoa
mwito kwa wananchi kuacha tabia ya kulifanya suala la upandaji miti kama
sherehe ama la msimu bali lifanywe kuwa endelevu na la kudumu.
Dkt. Mahenge
ametoa kauli hiyo baada ya kuongoza kazi
ya upandaji miti katika viunga vya
Hospitali ya Uhuru, wilayani Chamwino,
Mkoa wa Dodoma leo.
“Nataka
nitoe huu ujumbe kwamba, wakati wote tusilichukulie
hili zoezi la upandaji miti kama la kisherehe ama la misimu, nataka liwe
endelevu, liwe la kila siku hasa wakati wa msimu wa masika,”alisema Dkt.
Mahenge.
“Tusifanye kama
kulipangia tarehe fulani, mwezi Fulani
au siku fulani , hapana ikifika wakati wa masika kila mmoja apande miti, kwani
kazi ya kuokoa mazingira ni yetu sote,”amesisitiza Dkt. Mahenge.
Dkt. Mahenge
amewashukuru watu wote walioshiriki katika kazi hiyo ya upandaji miti, wakiwemo
wanafunzi 200 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Kitivo cha Elimu (COED) ambao
walimfuata ofisini kwake na kumuomba ashiriki nao kupanda miti eneo la
Hospitali ya Uhuru, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais John
Magufuli ya kuijenga hospitali hiyo kwa gharama ya sh. Bilioni 4.
Awali, Mkuu
wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga, alimshukuru Mkuu wa Mkoa, Dkt. Mahenge
kuhamasisha wanafunzi wa Udom kwenda kuungana na wananchi siku ya Sikukuu ya
Mapinduzi Zanzibar, kupanda miti kwa
lengo la kuthamini mchango mzuri wa Rais
Magufuli wa kuwajengea wananchi Hospitali ya Uhuru.
Naye, Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy amesema
kuwa siku hiyo ni njema na yenye baraka kwa
maana ya kuadhimisha Sikukuu ya Mapinduzi
ya Zanzibar sambamba na kupanda Zaidi ya
miti 500 na kuifanya Dodoma kuwa ya
kijani
.
Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM), Kitivo cha Elimu, Godfrey Masele, amesema kuwa wako
tayari muda wowote kushiriki katika
mapinduzi makubwa ya nchi yanayoendelea
chini ya uongozi wa Rais John Magufuli na kwamba watakuwa tayari pia muda wote
kushiriki kupanda miti kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Edson Sweti
aliwashukuru wote walioamua kuungana na wananchi wa Chamwino kwenda
kupanda miti katika eneo hilo ambalo pia ni makazi ya Rais Magufuli na kuahidi
kuitunza miti hiyo ili istawi vizuri.
Wakati huo
huo, Zaidi ya wanafunzi 80 wa Udom baada ya kumaliza kupanda miti, walishiriki
kuchangia damu katika Hospitali ya Uhuru ambayo imeanza kufanya kazi tangu
Desemba 21, 2020.
Kabla ya
kuanza kuchangia damu, wanafunzi hao walipatiwa elimu juu ya umuhimu wa suala
hilo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Damu Salama Hospitali ya Mkoa wa
Dodoma, Leah Kitundya.
Mdau karibu usikilize video hii ujue kilichozungumzwa...
IMEANDALIWA NA;
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇