Mwenyekiti wa Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT), Dk. Gaudentia Kabaka, akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Shule ya Awali iliyojengwa na Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Dodoma eneo la Kilimani, jijini Dodoma Desemba 19, 2020. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT Tanzania, Queen Mlozi, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Dkt Kabaka akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo
Dk. Kabaka akizungumza jambo na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule.
sehemu ya jengo la maduka lililozinduliwa ambalo limejengwa kwa gharama ya sh. milioni 51.
Sehemu ya maduka ambayo Mwekezaji Ismail Chande amefungua ofisi ya uchapishaji wa stika mbalimbali.
DKT Kabaka akikata utepe kuzindua rasmi jengo la maduka lililojengwa eneo la Kilimani, jijini Dodoma.
Dkt Kabaka akifunua pazia jiwe la msingi la jengo hilo la maduka
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma Neema Majule akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo.
Majule akipongezwa na Dk. Kabaka kwa uwekezaji wa kitega uchumi hicho
Katibu Msaidizi wa UWT Mkoa wa Dodoma, akipongezwa na Dk. Kabaka baada ya kusoma taarifa ya miradi hiyo.
Mwekezaji ambaye amejenga kwa ubia jengo la maduka kwa gharama ya sh. milioni 51, Ismail Chande akielezea mafanikio ya ujenzi huo. Kushoto kwake ni mkewe Chande.
Mbunge wa Viti Maalumu, Msanii Keisha akiimba wimbo wake wa Super Woman wakati wa hafla hiyo.
Sehemu ya wanawake wa CCM Mkoa wa Dodoma wakiwa katika hafla hiyo.
Wakicheza kwa fura wimo wa Msanii Keisha wa Super Woman
Mwalimu wa Shule ya Awali ya UWT Dodoma, akielezea umuhimu wa wazazi kuwapeleka watoto kwenye shule hiyo
Dk. Kabaka akikata keki iliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya hafla hiyo.
Dkt Kabaka akilishwa keki na Majule
Queen akilishwa keki na Majule
Mbunge wa Dodoma mjini akilishwa keki
Dk. Kabaka akifurahia zawadi ya kitenge aliyopatiwa na UWT Mkoa wa Dodoma
Dkt. Kabaka akikabidhiwa zawadi ya mchele kilo 50
Majule akigawa keki kwa madiwani wa viti maalumu pamoja na iongozi mbalimbali wa UWT
Wakipatiwa keki iliyoandaliwa maalumukwa ajili ya hafla hiyo.
Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma
Mwenyekiti wa Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT-CCM), Dk. Gaudentia Kabaka, ameupongeza uongozi wa
UWT Mkoa wa Dodoma kujenga vitega uchumi
vya mabanda ya maduka na shue ya Chekechea eneo la Kilimani, jijini Dodoma.
Kabaka alitoa pongezi hizo baada ya kuzindua rasmi vitega
uchumi hivyo, viliyogharimu zaidi y ash. Milioni 93, ambapo jengo la maduka
matano ambao ujenzi wake umegharimu sh mili. 51 na shule ya Awali sh. Milioni
42.2.
Jengo la maduka ambalo limejengwa kwa ubia na mwekezaji
Ismail Chande kwa makubaliano ya UWT kumkata pango la kila mwezi kwa muda wa miaka mitano mkataba utakapoisha. kwa mwezi mradi huo utakuwa unawaingizia sh.
milioni 12 na mradi wa shule utawaingizia takribani sh. milioni 100 kwa
mwaka.
Aidha Kabaka amempongeza
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule kwa uongozi wake imara
uliosababisha ujenzi wa vitega uchumi hivyo muhimu katika jamii kukamilika na
kuanza kufanya kazi.
Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa, Dkt Kabaka alisema kuwa kItendo hicho cha kishujaa kilichofanywa na wanawake wa Dodoma ni mfano mzuri na inatakiwa kiigwe na wanawake wa UWT nchi nzima, na kwamba maendeleo hayo atayatangaza popote atakapokwenda kwenye ziara za kikazi.
Jengo la shule hiyo ya Awali lililogharimu sh. milioni 42.2, limejengwa kwa michango mbalimbali wadau ambao ni; asilimia 10 ya michango ya madiwani wa viti maalumu sh. milioni 7.4, CCM Mkoa sh. milioni 8, wadau sh. milioni 7, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule sh. milioni 19.8. Pia baadhi ya wabunge, madiwani, watu binafsi na DUWASA walichangia,
Dk. Kabaka amewaonya watendaji watakaosimamia miradi hiyo vibaya ameapa kuwachukulia hatua za kisheria, lakini vile vile atawalaani na kusisitiza kwamba laana yake ni kubwa.
Jamani nampongeza Sana Neema majule na uwt mkoa was Dodoma kwa kazi nzuri walio ifanya,ccm oyeeeeer
ReplyDelete