LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 18, 2019

RAIS MAGUFULI AMETUSHIKA MKONO AKINAMAMA

       Tusimuangushe Rais Magufuli, akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza  Kuu  la Kamati ya Wanawake TUGHE Taifa uliofanyika Desemba 18, 2019 katika Ukumbi wa Edema Mkoani Morogoro. 

Katibu Kamati za Wanawake TUGHE Taifa Janejelly James ambaye alisema;  anakuwa Katibu kwa kupigiwa kura na Mkutano Mkuu wa Wanawake Taifa hiyo inampa sifa yakuwa mjumbe wa KUBK Taifa, Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa pia Mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu TUCTA Taifa.,


Akizungumzia kazi za kamati ya Wanawake ni  kuzungumzia  mambo yote yanayo wahusu watumishi wanawake ndani ya Serikali, Changamoto zao, Maendeleo yao, nakile ambacho watataka Serikali ifanye juu yao,


Tukisha yajadili tunayawakilisha katika Baraza Kuu la chama ambacho ni TUGHE na Baraza kuu ndio wenye mamlaka ya kukubali ya wasilishwe kwenye mkutano Mkuu wa chama ili yafanyiwe kazi.


Kwa majukumu yangu mengine nikuunganisha wanawake kwa kuleta mahusiano mema mahala pa kazi na kushauri  viongozi wetu kuwasemea wanawake watumishi katika ngazi za maamuzi ili wapewe nafa.


Ambapo Kwa hakika tunamshukuru Rais wetu Mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli kwa jinsi alivyowateua kwenyenafasi mbalimbali za kimaamuzi watumishi wanawake.



Kwa kitendo cha kumteua Makamu wake mama samia kwetu ni faraja sana, Naibu Spika, Mawaziri na hasa Mama jenista Muhagama ambaye yupo karibu na vyama vya wafanyakazi 



Hakika tunawanawake wetendadaji wengi Makatibu Wakuu, tunawanawake Watunga sera, Mawaziri wapo, Wakurugezi waidara mbalimbali na ninaishukuru Serikali kwa ujumla kwa kutuona wanawake katika Teuzi mbalimbali.        

Afisa Elimu Kazi na Mratibu wa Jinsia TUGHE Nsubisi Mwasandende, akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo alianza kwa kusema; Tupo hapa mkoani Morogoro katika majukumu ya kazi ambapo tumeanza vikao vya Matawi, Baraza la TUGHE  Vikao vya Kamati Tendaji na tupo katika Baraza la Wafanyakazi.

Baraza Kuu la Wafanyakazi na tutamalizia na Mkutano Mkuu wa Chama na moja kati ya hoja tunazo jadili ni Taarifa ya Chama chetu ndani ya miaka miwili na Nusu kwa mujibu wa Katiba yetu, kila baa ya muda huo hutoa taarifa, changamoto gani tumepitia jumla kuangalia changamoto za Watumishi wa Umma, Maendeleo ya Chama na ustawi wa wanachama wetu kwa ujumla ikiwemo Marekebisho ya Katiba ya Chama.

 Sisi kama TUGHE tunaamini ndicho Chama Kikubwa na tunataka kuwa chama Cha mfano Tanzania nzima ili vyama vingine kuiga mfano kutoka kwetu ili vyama vingine vijifunze Demokrasia mahala pa kazi.

Tupo katika kujadiliana maendeleo ya Utumishi wa Umma na ushiriki katika maswala ushiriki swala zima la Demokrasia na kuishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Tano kwa maana imeendelea kuruhusu na kutoa uhuru vyama vya wafanyakazi na kujadili mambo yao na tunashukuru pia kwa kuleta maendeleo kwa Wananchi ambayo yatakuwa na chango chanya na tunawatakia heri viongozi wote wa Serikali ya Awamu ya Tano na na kuwatakia heri watumishi wote wa Umma na tukumbuke wafanyakazi ndio nguzo muhimu katika uchumi wa nchi

 MwenyekitiTUGHE Mkoa wa Pwani, Catherine Katele alianza kwa kumshukuru Mungu kwa Kuwezesha kwa wajumbe kuhudhuri kikao kinachoendele hapa Mkoani Morogoro nawajumbe wamefika wakiwa na Afya nzuri na tunawakilishana vizuri na tunaongea mabo mengi ya wafanyakazi alisema Katele; 

Pia napenda kuishukuru Serikali ya Tanzania hasa kwa kipindi hiki cha awamu ya Tano ikiongozwa na Jemedari wa Mapambano anayepigania wanyonge ambaye ametusaidia sana vyama vya wafanyakazi, kwakuhimiz mabaraza ya wafanyakazi kuweza kufanyika sehem za kazi

Hii imetusaidia kwa wafanyakazi kujuwa umuhim wa vyama vya wafanyakazi, tumekuwa tukifanya mabaraza ya wafanyakazi huku tukiibua matatizo mengi ambayo wafanyakazi walikuwa wakiogopa kupoteza ajira zao lakini Rais wetu amekuwa muuungwana na amekuwa akipenda kituhiki kiwe wazi

Ofisi zote na wanachama wote wanaofanya kazi Tanzania wana Mabaraza na wanamabaraza mahala pa kazi japo yapo maeneo machache yanajitahiidi hili kwa pamoja, kwahiyo mimi ninapenda kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuhimiza hili kwa wafanyakazi  


 Katibu Mkuu TUGHE Hery Mkunda akipokea Rambirambi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti Margareth Kajuju kwa niaba ya Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama hicho John Sanjo aliyefiwa na mama yake, kuanzia kushoto ni Katibu Kamati ya Wanawake TUGHE Taifa Janejelly James na Dr, Jane Madete Mwenyekiti Kamati ya Wanawake TUGHE.
Makamu Mwenyekiti Magre Kajuju akimkabidhi  Sabina Massawe Rambirambi mara baada ya kufiwa na mama yake

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages