Feb 13, 2019

MWIGULU NCHEMBA ASIMULIA WALIVYOPATA AJALI

Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, amesema chanzo cha ajali aliyopata ni dereva kukwepa punda watatu.

Ajali hiyo ilitokea leo Jumatano Februari 13, katika eneo la Migori Mkoani Iringa akiwa safarini kuelekea Singida kuhudhuria kikao cha kamati ya siasa ya mkoa.

“Punda walikuwa wanavuka barabara sasa dereva wangu akajaribu kuwakwepa lakini ikashindikana, baada ya hapo nilisikia kishindo kikubwa na moshi umetanda ndani ya gari, ilikuwa imepinduka.

“Wasamaria wema wakaja kutuchukua na kutuleta hapa hospitalini, lakini namshukuru Mungu kutoka mzima kwani mkanda ulikuwa umenibana sana,” amesema. 

Mwigulu amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma akiendelea na matibabu




Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba1 amepata ajali ya gari akiwa njiani barabara ya Iringa kuelekea Dodoma na amekimbizwa hospitali ya Dodoma. 






No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages