Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema Maandalizi ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuharakisha upatikanaji umeme kwa Waafrika milioni 300 ifikapo 2030 (Mission 300) yamefikia asilimia 95 na kazi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na kukamilisha ukarabati wa ukumbi wa JNICC, usajili na uthibitisho wa wageni watakaokuja na ukarabati wa maeneo mengine yatakayotumika kwenye mkutano huo.
"nichukue nafasi hii kuupongeza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa hatua iliyofikiwa na kuliweka jiji kwenye mandhari ya kuvutia.” akasema Dk. Biteko.
Dk. Biteko ameyasema hayo leo Januari 15, 2025, katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, baada ya kukagua maandalizi kwenye ukumbi huo ambako mkutano huo utafanyika mwishoni mwa mwezi huu (Januari 27 na 28).
Amesema Mkutano huo umekuwa kivutio duniani kushawishi Wakuu wa Taasisi nyingi za Kimataifa kuonyesha nia ya kushiriki mkutano huo mkubwa katika Sekta ya Nishati.
Kuhusu Tanzania kuteuliwa kwaTanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo pamoja na mambo mengine lakini kuwa zaidi kumetokana na Diplomasia nzuri ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambayo imezidi kuimarisha uhusiano wa Tanzania Kimataifa na kufanya Benki ya Dunia (WB) na na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano.
Dk. Biteko ambaye aliambatana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila. amesema Wakuu wa Nchi 54 kutoka Bara la Afrika na viongozi wengine watakaoshiriki mkutano huo ni Mawaziri wa Fedha na Nishati kutoka barani Afrika, Marais wa Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), pamoja viongozi kutoka Jumuiya ya Ulaya (EU) na Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU).
Ametaja sababu nyingine ya Tanzania kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo muhimu mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya Nishati huku akitoa mfano wa mafanikio katika usambazaji wa nishati vijijini.
Amesema vijiji vyote nchini 12,318 vimesambaziwa umeme na Vitongoji 34,000 kati ya 64,274 vilivyopo nchini, tayari vimesambaziwa
umeme.
Ametaja baadhi ya faida za mkutano huo kuwa ni pamoja na kuongezeka idadi ya Watanzania watakaounganishwa na umeme ifikapo mwaka 2030 hadi kufikia milioni 13.5 kutoka milioni 5.2 ya sasa.
Ameongeza kuwa, katika mkutano huo nchi zitasaini mikakati ya kuharakisha kusambaza umeme kwa wananchi ambayo itaeleza kwa kina
hatua gani zitachukuliwa chini ya mwavuli wa WB na AfDB.
Ameongeza kuwa, faida nyingine zitakazotokana na mkutano wa M300 ni kuongezeka kwa fursa za uwekezaji, kuimarisha biashara na kuongeza heshima ya nchi katika Duru za kimataifa na Tanzania kuwa Taifa linalopigiwa mfano kwenye nyanja mbalimbali.
Dkt. Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuupokea kwa mikono miwili mkutano huo ambao kwa kiasi kikubwa unazidi kumheshimisha Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan na Watanzania kwa ujumla.
Aidha, ametoa mwito kwa wananchi kuendelea na hali ya amani na utulivu kuelekea katika mkutano huo wa kihistoria kutoka nchi ipige hatua kwenye Sekta ya Nishati kwani ni Mkutano Mkubwa wa kwanza kufanyika.
Vilevile ametoa mwito kwa Waandishi wa Habari kuutangaza Mkutano huo kwa Watanzania ili waufahamu kwa kina na kufahamu fursa zilizopo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema maandalizi ya kupokea ugeni huo yako katika hatua za mwisho, na kuongeza kuwa ili kufanikisha mkutano huo, baadhi ya mitaa itafungwa ili kuwezesha maonesho na utalii wa ndani ikiwa ni pamoja na utalii wa tiba.
Your Ad Spot
Jan 15, 2025
Home
featured
Kitaifa
DK. BITEKO: MAANDALIZI YA MKUTANO WA NISHATI WA WAKUU WA NCHI AFRIKA YAFIKIA ASILIMIA 95, UMEKUWA KIVUTIO DUNIANI
DK. BITEKO: MAANDALIZI YA MKUTANO WA NISHATI WA WAKUU WA NCHI AFRIKA YAFIKIA ASILIMIA 95, UMEKUWA KIVUTIO DUNIANI
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About Bashir Nkoromo
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇