LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 9, 2018

AKINA MAMA 30 HUPEZA MAISHA KILA SIKU KUTOKANA NA CHANGAMOTO ZA UZAZI NCHINI TANZANIA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezindua kampeni maalumu ya kukabiliana na changamoto za kiafya kwa akina mama hasa wakati wa kujifungua.
Kampeni hiyo iliyopewa jina la  "Jiongeze, tuwavushe salama" imezinduliwa Mkoani Dodoma na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Bi Samia Suluhu Hassan.
Kampeni hiyo imezinduliwa huku ripoti mbalimbali za afya zikionyesha uwepo wa vifo vya akina mama wakati wa kujifungua katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Uzinduzi wa kampeni hii unakuja wakati ikikadiriwa kuwa, wanawake 11, 000 hupotezsa maisha kila mwaka nchini Tanzania wakati wa kujifungua idadi ambayo ni sawa na kuaga dunia kila siku wanawake 30.  
Mama akifurahia kichanga chake baada ya kujifungua salama
Aidha ripoti zinasema kuwa, ni asilimia 40 tu ya wanawake wajawazito ndio ambao huhudhuria kliniki na katika vituo vya afya wakati wakiwa wajawazito kwa ajili ya kuangalia afya na maendeleo yao katika kipindi hicho cha ujauzito.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, kampeni iliyozinduliwa inalenga kuongeza msukumo kwa serikali na wadau wengine wa afya kuongeza uwajibikaji ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi wa watoto wachanga pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili akina mama wakati wa kujifungua.
Raia wengi wa Tanzania wanaishi katika maeneo ya vijijini ambako bado huduma za afya si za kuridhisha na kulifanya suala hilo kuwa moja ya changamoto muhimu mno kwa jamii ya Watanzania yenye wakazi milioni 57.33 kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages